Waethiopia elfu 3 wakimbilia Sudan wakihepa vita katika eneo la Tigray
(last modified Thu, 29 Jul 2021 02:32:47 GMT )
Jul 29, 2021 02:32 UTC
  • Waethiopia elfu 3 wakimbilia Sudan wakihepa vita katika eneo la Tigray

Vyombo vya habari vimetangaza kuwa, wakimbizi wa Kiethiopia zaidi ya elfu tatu wamewasili Sudan katika kipindi cha siku moja tu kufuatia mapigano yanayoendelea huko Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Shirika rasmi la habari la Sudan limeripoti kuwa, viongozi wa kieneo katika mkoa wa al Qadarif mashariki mwa nchi hiyo wamewapokea na kuwapa makazi ya muda wakimbizi wa Kiethiopia wapatao elfu tatu ambao wamekimbia mapigano kaskazini mwa Ethiopia. 

Idadi hiyo ya wakimbizi wa Kiethiopia imetajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kuwasili katika ardhi ya Sudan tangu mwezi Novemba mwaka jana baada ya kuanza mapigano kati ya jeshi la Ethiopia na waasi wa Harakati ya Ukombozi ya Eneo la Tigray (TPLF). 

Waasi wa eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia 

Hadi kufikia sasa wakimbizi wa Ethiopia elfu 78 wamevuka mpaka wa nchi yao na kuingia Sudan.

Mapigano kati ya serikali jeshi la ya Ethiopia na waasi wa harakati ya TPLF yalianza mwezi Novemba mwaka jana. Hadi sasa mapigano hayo yamewalazimisha watu karibu milioni mbili kuwa wakimbzi na wengine laki nne kukabiliwa na hali ngumu na ukosefu wa chakula. 

Tags