Buhari: Mauaji ya wasafiri wa Kiisilamu yalikuwa yamepangwa mapema
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i73540-buhari_mauaji_ya_wasafiri_wa_kiisilamu_yalikuwa_yamepangwa_mapema
Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa, mauaji ya watu 23 waliokuwa wakirudi kutoka kwenye sherehe ya Waislamu nchini Nigeria lilikuwa shambulio la kukusudia na kupangwa na kwamba watuhumiwa wa mauaji hayo tayari wamekamatwa.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 15, 2021 06:26 UTC
  • Muhammadu Buhari
    Muhammadu Buhari

Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa, mauaji ya watu 23 waliokuwa wakirudi kutoka kwenye sherehe ya Waislamu nchini Nigeria lilikuwa shambulio la kukusudia na kupangwa na kwamba watuhumiwa wa mauaji hayo tayari wamekamatwa.

Katika taarifa yake ya leo, Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amelaani shambulio hilo la Jumamosi ililolenga mabasi yaliyokuwa yamebeba Waislamu waliokuwa wakirejea makwao baada ya kushiriki katika shughuli ya kidini katika Jimbo la Plateau.

Buhari amesema: "Ni wazi hili lilikuwa shambulio lililopangwa mapema kwa shabaha iliyojulikana awali, na kutokana na imani ya kidini wa wasafiri hao.

Rais wa Nigeria ameongeza kuwa, hilo ni shambulio la moja kwa moja lililofanyika kwa nia mbaya kwa wanajamii wanaotumia haki yao ya kusafiri kwa uhuru na kufuata imani ya chaguo lao.

Gavana wa Jimbo la Plateau, Simon Lalong amesema vyombo vya usalama vimekamata washukiwa 20 na imetangaza marufuku ya kutoka nje kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni katika eneo hilo kwa sababu ya hofu ya machafuko ya kulipiza kisasi.

Amesema hiki ni kitendo cha kihalifu na jinai ambayo haipaswa kupewa sifa ya kabila au dini maalumu. 

Katika miaka ya karibuni Nigeria imekumbwa na machafuko makubwa ya kikabila na hujuma za kigaidi za kundi la Boko Haram ambazo zimesababisha mauaji ya maelfu ya raia wasio na hatia yoyote.