Jeshi la Sudan lakadhibisha kuwepo juhudi za kufanya mapinduzi nchini humo
(last modified Mon, 13 Sep 2021 03:07:08 GMT )
Sep 13, 2021 03:07 UTC
  • Jeshi la Sudan lakadhibisha kuwepo juhudi za kufanya mapinduzi nchini humo

Jeshi la Sudan limetoa taarifa na kukanusha kuwepo jitihada za aina yoyote za kufanya mapinduzi nchini humo.

Jeshi la Sudan jana Jumapili limekadhibisha taarifa zilizotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba wanajeshi wa nchi hiyo walikuwa wakifuatilia jitihada za kufanya mapinduzi huko Sudan; na kwa mara nyingine tena limetangaza kuheshimu na kufungamana na wajibu wake wa kuilinda nchi na serikali ya mpito ya nchi hiyo.  

Taarifa zilizotolewa na tovuti mbalimbali za habari za Sudan na katika mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa jeshi la Sudan limegundua njama zilizopangwa za kufanya mapinduzi nchini humo. 

Maandamano ya wananchi dhidi ya serikali ya raia wa wakati huo Omar al Bashir yalianza kushuhudiwa Sudan tangu Disemba mwaka 2018. Rais al Bashir aling'olewa madarakani mwezi Aprili mwaka 2019 na sasa Sudan inaongozwa na serikali ya mpito.  

Omar al Bashir, Rais wa zamani wa Sudan aliyeng'olewa madarakani  

 

Tags