Siku ya Afrika inaadhimishwa leo mjini Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7777-siku_ya_afrika_inaadhimishwa_leo_mjini_tehran
Sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika zinafanyika leo hapa mjini Tehran katika ofisi ya utafiti wa kisiasa na kimataifa ya Wizara ya Mambo ya Nje.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 25, 2016 07:31 UTC
  • Siku ya Afrika inaadhimishwa leo mjini Tehran

Sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika zinafanyika leo hapa mjini Tehran katika ofisi ya utafiti wa kisiasa na kimataifa ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Sherehe hizo zinafanyika kwa kuhudhuriwa na maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na mabalozi wa kigeni walioko hapa nchini hususan wa nchi za Afrika.

Tarehe 25 Mei imetangazwa kuwa Siku ya Afrika. Katika siku kama ya leo mwaka 1963, Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) uliasisiwa, ambapo siku hiyo viongozi wa nchi 30 kati ya 32 za Kiafrika zilizokuwa zimepata uhuru wakati huo walisaini Hati maalumu katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Mwaka 2002, Umoja wa Nchi Huru za Afrika ulibadilisha jina lake na kuitwa Umoja wa Afrika (AU).../