Polisi ya Nigeria yadai kukomboa mateka 94 kutoka kwa magenge ya wahalifu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i79928-polisi_ya_nigeria_yadai_kukomboa_mateka_94_kutoka_kwa_magenge_ya_wahalifu
Polisi ya Nigeria imetangaza kuwa watu 94 wameokolewa baada ya kuchukuliwa mateka na makundi yenye silaha katika majimbo ya Zamfara, Niger na Katsina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2022 04:34 UTC
  • Polisi ya Nigeria yadai kukomboa mateka 94 kutoka kwa magenge ya wahalifu

Polisi ya Nigeria imetangaza kuwa watu 94 wameokolewa baada ya kuchukuliwa mateka na makundi yenye silaha katika majimbo ya Zamfara, Niger na Katsina.

Kinyume na madai ya Rais Mohammadu Bohari wa Nigeria ya kupambana na ugaidi, makundi yenye silaha na magenge ya wahalifu nchini Nigeria yamekuwa yakishambulia vijiji na kuua watu ovyo, na wakati mwingine wanavijiji wamekuwa wakichukuliwa mateka kwa shabaha ya kutumiwa kwa ajili ya kuomba vikomboleo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, maafisa wa polisi wa Nigeria wanasema, manusura wa utekaji nyara wa makundi yenye silaha katika majimbo ya Zamfara na Katsina, na Niger, magharibi mwa Nigeria, wanapatiwa matibabu na baadaye watakabidhiwa kwa familia zao.

Taarifa ya Polisi ya Nigeria imesema, 32 kati ya waliookolewa kutoka mikononi mwa makundi yenye silaha walikuwa wanawake. 

Zaidi ya watu 50 wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya waasi kwenye vijiji kadhaa katika jimbo la Zamfara nchini Nigeria.