Wanaigeria wazuiwa kwenda kupigana vita Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i81128-wanaigeria_wazuiwa_kwenda_kupigana_vita_ukraine
Serikali ya Nigeria imesema kuwa haitamruhusu raia wake yoyote kwenda kupigana vita Ukraine baada ya Russia kuishambulai nchi hiyo hivi karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2022 08:58 UTC
  • Wanaigeria wazuiwa kwenda kupigana vita Ukraine

Serikali ya Nigeria imesema kuwa haitamruhusu raia wake yoyote kwenda kupigana vita Ukraine baada ya Russia kuishambulai nchi hiyo hivi karibuni.

Nigeria imetamka hayo baada ya ripoti kudai kuwa, baadhi ya raia wa Nigeria wamejitolea kwenda kupigana nchini Ukraine kuiunga mkono serikali ya Kiev dhidi ya Russia. Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imeeleza kuwa, Ubalozi wa Ukraine umekanusha kuhusika kivyovyote vile na zoezi hilo tajwa.

Hata hivyo ubalozi huo umethibitisha kuwa, raia kadhaa wa Nigeria waliuomba ubalozi huo wakionyesha nia yao ya kujiunga vitani huko Ukraine. Wakati huohuo ubalozi wa Ukraine umejiweka mbali na madai kwamba, ulikuwa ukimuomba kila raia wa Nigeria kiasi cha dola elfu moja mwenye lengo la kujiunga vitani huko Ukraine kwa ajili ya kugharamia tiketi ya ndege na viza. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria amesema kuwa, Abuja inapinga kutumiwa mamluki popote pale duniani na haitavumilia kuajiriwa raia wowote nchini kwake au kutumiwa wananchi wa Nigeria kama vibaraka kupigana vita huko Ukraine au sehemu nyingine yoyote duniani. Nigeria imetangaza wazi msimamo wake huo siku kadhaa baada ya Senegal kuwaonya raia wa nchi hiyo wanaotaka kujitolea kwenda kupigana vita huko Ukraine dhidi ya Russia.  

Mashambulizi ya Russia dhidi ya Ukraine