Genge lenye silaha lashambulia kambi ya wakimbizi nchini Sudan
Genge moja lenye silaha limevamia na kushambulia kambi moja ya wakimbizi katika jimbo la Darfur la magharibi mwa Sudan na kuua na kujeruhi watu wasiopungua 7.
Shirika la habari la Tasnim limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kundi moja la watu wenye silaha limeivamia kambi ya wakimbizi ya Kalama ya kusini mwa jimbo la Darfu wakati yalipokuwa yanafanyika mashindano ya mpira wa mikuu na kuua wachezaji watatu wa mpiga na kujeruhi wengine wanne.
Jimbo la Daruf limekumbwa na mapigano baina ya askari wa serikali na waasi wenye silaha tangu mwaka 2003 na takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu laki tatu wameshauwa na wengine milioni mbili na laki tano wamekuwa wakimbizi kutokana na mapigano hayo.
Mapigano katika jimbo la Darfur yameongezeka kwenye miaka ya hivi karibuni kutokana na mashambulizi ya magenge ya wanamgambo wenye silaha na baadhi ya wakati huwa ni kutokana na uadui mkubwa uliopo baina ya makundi hasimu.
Hivi karibuni pia, kundi moja lenye silaha liliua watu wawili wa kabila moja la Waarabu huko magharibi mwa Darfur. Mauaji hayo yalizusha mapigano makubwa ya kikabila ya umwagaji damu na kupelekea watu wasiopungua 270 kuuawa na wengine 20,000 kuyakimbia makazi yao.
Tarehe 25 Novemba mwaka jana pia, Umoja wa Mataifa ulitangaza habari ya kuuawa watu 43 na kutokea moto kwenye vijiji 46 baada ya kuzuka mapigano baina ya makabila hasimu ya jimbo hilo la Darfur la magharibi mwa Sudan.