Idadi ya watu waliouawa katika mapigano ya kikabila Sudan yafikia 100
(last modified Mon, 13 Jun 2022 07:58:03 GMT )
Jun 13, 2022 07:58 UTC
  • Idadi ya watu waliouawa katika mapigano ya kikabila Sudan yafikia 100

Imeelezwa kuwa, idadi ya watu waliouawa katika mapigano ya kikabila ya hivi karibuni huko Darfur magharibi Sudan imeongezeka na kufikia wahanga 100.

Gazeti la al-Rakoba la Sudan limeripoti kuwa, miili kadhaa iliyochomwa moto imepatikana ikiwa imetapakaa katika vijiji vya maeneo hayo ya magharibi mwa Sudan

Ripoti zinasema kuwa, jumla ya mili 62 imepatikana katika vijiji mbalimbali vya magharibi mwa Sudan huku makumi ya watu wengi wakiwa hawajulikana walipo tangu mapigano hayo yalipozuka tena juma lililopita.

Machafuko hayo yanaripotiwa huku Sudan ikiwa imegubikwa na wimbi la machafuko yaliyosababishwa na mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba mwaka uliopita yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Ripoti zinasema, katika jimbo la Darfur Magharibi linalopakana na Chad, mapigano yalizuka karibu na Kolbus, eneo lililoko umbali wa kilomita 160 kutoka El Geneina, makao makuu ya jimbo hilo, ambapo washambuliaji waliviteketeza kwa moto vijiji vya eneo hilo.

Watoto wa Darfur ndio wahanga wakuu wa machafuko katika jimbo hilo la magharibi mwa Sudan

 

Inaelezwa kuwa, awali mapigano ya kugombea ardhi yalizuka baina ya watu wa kabila la Waarabu na mkulima mmoja wa jamii hiyo ya wasio Waarabu na kusababisha watu wanane wa jamii ya Gimiri kuuawa na vijiji vitatu kuchomwa moto.

Huko Kordofan Kusini pia mapigano yamezuka baina ya jamii mbili za makundi hasimu ya Waarabu ya Hawazma na Kenana.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes anikuliwa hivi karibuni akisema kuwa, wasiwasi mkubwa na mapigano ya kikabila yaliyozuka katika jimbo la Kordofan Kusini.

Tags