Watu saba wauawa na kujeruhiwa Kenya
Mapigano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji katika mji wa Kisumu Kenya yamesababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine sita.
Habari zinasema kuwa maandamano ya mitaani yaliyofanywa na wakazi wa mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya ambayo ni makuu makuu ya muungano wa upinzani wa CORD yamesababisha kutokea mpambano kati ya wafanya maandamano na vikosi vya usalama. Mapigano hayo yalijiri jana Jumatatu katika mji wa Kisumu wakati vikosi vya usalama na polisi wa kuzuia ghasia walipojaribu kuzima maandamano hayo.
Watu wengi walioshuhudia ghasia hizo wameeleza kuwa mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi moja kwa moja na polisi.
Wafanya maandamano hao walifunga barabara, kuchoma moto vitu mbalimbali na kuwarushia mawe polisi huku wakitaka ifanyiwe marekebisho Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo.
Hii ni katika hali ambayo kwa kuzingatia kuongezeka wimbi la ukosoaji kwa polisi wa Kenya katika kuamiliana na waandamanaji, Mkuu wa Polisi wa nchi hiyo ameagiza kuanza uchunguzi kuhusu suala hilo. Maandamano hayo kote nchini Kenya yamefanyika kufuatia wito uliotolewa na Raila Odinga Mkuu wa Muungano wa vyama vya upinzani CORD, ambaye alishindwa na Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2013.