Al-Burhan: Taasisi za kiraia zisiingilie masuala ya jeshi la Sudan
(last modified Thu, 08 Sep 2022 02:50:59 GMT )
Sep 08, 2022 02:50 UTC
  • Al-Burhan: Taasisi za kiraia zisiingilie masuala ya jeshi la Sudan

Mkuu wa baraza tawala la Sudan ameonya kuhusu uingiliaji wowote wa makundi ya kiraia ya nchi hiyo katika taasisi ya kijeshi.

Abdel Fattah al-Burhan ambaye pia ni kamanda mkuu wa vikosi vya jeshi la Sudan, almesema: "Baadhi ya watu wanajaribu kuanzisha fitina na hitilafu kati ya jeshi na vikosi vya radiamali ya haraka." Amesisitiza kuwa, vikosi hivyo vya jeshi havitatumia silaha zao dhidi ya kila mmoja wao na kwamba hakuna mtu mwenye haki ya kuingilia masuala ya jeshi.

Al-Burhan amesisitiza kuwa, makundi ya kiraia yanapaswa kufuatilia suala la makubaliano na kuunda serikali mpya, badala ya kuzusha fitina kati ya taasisi za kijeshi.

Mkuu wa baraza tawala la Sudan amesisitiza udharura wa kuendelezwa juhudi za kulindwa taasisi ya kijeshi hadi itakapoundwa serikali iliyochaguliwa, na kuongeza kuwa, vikosi vya jeshi vinafanya jitihada za kudumisha umoja wa nchi ya Sudan. 

Matamshi haya ya Jenerali Abdel Fattah al Burhan yametolewa baada ya kuchapishwa ripoti kadhaa kuhusu kuwepo kwa tofauti kati ya jeshi na vikosi vya radiamali ya haraka, na vilevile matakwa ya makundi ya kiraia ya Sudan ya kukarabatiwa muundo wa jeshi la nchi hiyo.

Tags