Viongozi wa nchi za Afrika wazitaka nchi tajiri kutekeleza ahadi zao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i87996-viongozi_wa_nchi_za_afrika_wazitaka_nchi_tajiri_kutekeleza_ahadi_zao
Wawakilishi wa nchi 24 za Afrika wamezitaka nchi zilizoendelea kutekeleza ahadi zao za kutoa msaada wa kifedha kwa bara la Afrika ilikukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 10, 2022 02:24 UTC
  • Viongozi wa nchi za Afrika wazitaka nchi tajiri kutekeleza ahadi zao

Wawakilishi wa nchi 24 za Afrika wamezitaka nchi zilizoendelea kutekeleza ahadi zao za kutoa msaada wa kifedha kwa bara la Afrika ilikukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.

Taarifa ya viongozi na wawakilishi wa nchi za Afrika walioshiriki mkutano wa awali wa mabadiliko ya tabianchi mjini Cairo, inaeleza kuwa: Tunaziomba nchi zilizoendelea kutimiza wajibu wao wa kifedha katika nyanja za hali ya hewa na maendeleo na ahadi zao za kuzidisha maradufu fedha kwa ajili ya nishati ya kijani, hasa barani Afrika.

Viongozi wa Afrika pia wamekumbusha athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa katika bara hilo, ikizingatiwa kuwa Afrika inachangia chini ya 4% ya uzalishaji wa gesi chafu.

Kulingana na tangazo la Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi kwa Afŕika, madhumuni ya mkutano huo ni kutoa ufadhili wa kusaidia nchi zilizo katika mazingira magumu zaidi kwa ajili ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

Katika hafla ya kufunga mkutano huo, Rania Al-Mashat, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Misri, alisema kuwa kwa nchi hiyo, kongamano hilo linatoa uwezekano wa kudhamini fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Maeneo ya pwani ya kaskazini mwa nchi ya Misri yenye idadi ya watu milioni 103, yanakabiliwa na tishio kutokana na kuongezeka kwa maji, na matumbawe ya maeneo hayo yanakufa kutokana na kupanda kwa joto katika Bahari Nyekundu.