Burkina Faso yaamuru kuondoka nchini humo mratibu wa UN; yasema haimkubali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i92088-burkina_faso_yaamuru_kuondoka_nchini_humo_mratibu_wa_un_yasema_haimkubali
Burkina Faso imeamuru kuondoka nchini humo Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa haimkubali mwanadiplomasia huyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 24, 2022 23:49 UTC
  • Burkina Faso yaamuru kuondoka nchini humo mratibu wa UN; yasema haimkubali

Burkina Faso imeamuru kuondoka nchini humo Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa haimkubali mwanadiplomasia huyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Burkina Faso imesema kuwa, wanamtangaza mwanadiplomasia huyo Muitalia Barbara Manzi kuwa shakhsia asiyekubalika nchini Burkina Faso, ambapo alitakiwa kuondoka nchini humo juzi Ijumaa.  

Olivia Rouamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso amesema uamuzi wa Barbara Manzi wa kuwaondoa kwa upande mmoja wafanyakazi  wa akiba wa UN kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Ouagadougou umehalalisha hatua hiyo. Amesema hatua iliyochukuliwa na Mratibu Mkazi wa UN inadunisha na kutia dosari taswira ya Burkina Faso na kuwazuia wawekezaji kuwekeza nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso ameonegza kuwa, Manzi alitabiri kujiri machafuko huko Burkina Faso katika miezi ijato na kwamba Umoja wa Mataifa unapasa kuchukua hatua kama chombo cha usaidizi wakati nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika ikipambana dhidi ya makundi ya kigaidi yenye silaha. 

Al Qaida ,Burkina Faso 

Burkina Faso ilitumbukia katika hali ya machafuko na mashambulizi ya makundi ya kigaidi tangu mwaka 2015. Mashambulizi hayo yanatajwa kufanywa na mtandao wa kigaidi wa al Qaida na kundi la Daesh. Maelfu ya watu wameuawa hadi sasa na wengine wasiopungua milioni mbili wamelazimika kuhama makazi yao kufuatia hujuma hizo za magaidi.