Al Burhan asisitiza vikosi vya ulinzi kujitoa katika shughuli za kisiasa
Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan amesisitiza kuhusu vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo kuachana na shughuli za kisiasa.
Mchakato wa kisiasa wa Sudan uliasisiwa Disemba 5 mwaka jana katika kalibu ya mfumo wa makubaliano ya kisaisa; ambapo kipengee muhimu zaidi cha makubaliano hayo ni kujitoa jeshi la nchi hiyo katika muundo wa kisiasa.
Kikao cha kuanza marhala ya mwisho ya mchakato wa kisiasa wa Sudan kimefanyika kwa kuhudhuriwa na pande tatu za Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Igad.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Jenerali Abdel Fattah al Burhan Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan amesisitiza azma ya jeshi la nchi hiyo ya kujiondoa katika muundo wa kisiasa na katika serikali ya baadaye na kutekeleza jukumu lake la kijeshi la kuilinda Sudan.
Yasser Arman mmoja wa viongozi wa Harakati ya Uhuru na Mageuzi ya Sudan pia amesema kuwa lengo la mchakato wa kisiasa wa Sudan ni kuanzisha jamii mpya na kupitisha kipindi cha mpito kutoka serikali ya chama kimoja na kuwa serikali ya kitaifa.
Katika upande mwingine, Mohamed Hamdan Dagalo Naibu Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan ameeleza kama ninavyomnukuu, "sisitizo letu ni kufanyia marekebisho taasisi za kijeshi na kuunda jeshi la taifa mbali na uingiliaji wowote wa kisiasa," mwisho wa kunukuu.
Wananchi wa Sudan wanaoandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum na katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wanaamini kuwa jeshi halitaondoka kikamilifu madarakani licha ya kufikiwa makubaliano hayo ya kisiasa, na ndio maana wanasisitiza kuendeleza maandamano nchini.