Lavrov aunga mkono takwa la Sudan la kuondolewa vikwazo vya UN
(last modified Fri, 10 Feb 2023 06:56:31 GMT )
Feb 10, 2023 06:56 UTC
  • Lavrov aunga mkono takwa la Sudan la kuondolewa vikwazo vya UN

Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amekutana na kufanya mazungumzo huko Khartoum mji mkuu wa Sudan na viongozi wa nchi hiyo na kuahidi kuunga mkono takwa lao la kuondolewa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo.

Ziara ya siku mbili ya Lavrov huko Sudan ni katika juhudi za Russia ya kuzidisha ushawishi wake barani Afrika kufuatia baadhi ya madola kufanya jitihada za kuitenga Moscow kimataifa kuafuatia oparesheni zake za kijeshi dhidi ya Ukraine. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amewaambia waandishi wa habar akiwa pamoja na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali al Sadiq kuwa; Moscow iko pamoja na Sudan katika juhudi zake za kutaka kuondolewa vikwazo dhidi ya nchi hiyo. 

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan aidha amesisitiza haja ya nchi mbili kushirikiana katika Umoja wa Mataifa ili kutilia makazo suala la kufanyika mageuzi ndani ya Baraza la Usalama la umoja huo. 

Hivi karibuni Sudan ilikariri wito wake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nchi hiyo kuondolewa vikwazo vya silaha na vinginevyo. Umoja wa Mataifa iliiwekea Sudan vikwazo wakati wa machafuko ya Darfur mwaka 2005.  

Sergei Lavrov jana alikuwa na mazungumzo na Abdul Fattah al Burhan mkuu wa baraza la uongozi la kijeshi la Sudan; ambaye mwezi Oktoba mwaka 2021 aliongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyovuruga mchakato wa Sudan wa kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia. Mapinduzi hayo yalipelekea nchi wafadhili kusitisha misaada yake kwa Sudan. 

Luteni Jenerali Abdel Fattah al Burhan 

 

Tags