Vijana waandamana dhidi ya safari ya Macron mjini Kinshasa
(last modified Thu, 02 Mar 2023 04:23:49 GMT )
Mar 02, 2023 04:23 UTC
  • Vijana waandamana dhidi ya safari ya Macron mjini Kinshasa

Makumi ya vijana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa jana waliandamana wakipinga ziara ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa nchini humo.

Wafanya maandamano hao ambao aghalabu yao ni vijana walikusanyika nje ya ubalozi wa Ufaransa huko Kinshasa huku wakipira nara" Macron muuaji na ondoka nchini" kwetu huku wakipeperusha bendera za Russia.

Kundi hilo la vijana wa Kikongo linamtuhumu Rais Emmanuel Macron kuwa anaiunga mkono na kutoa himaya kwa Rwanda; nchi inalaumiwa kutokana na  hali ya ukosefu wa amani inayoshuhudiwa mashariki mwa Kongo. 

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa 

Mratibu wa vuguvugu kwa jina la " Harakati ya Wananchi ya  Sang-Lumbumba ameeleza haya na hapa ninamnukuu" Rwanda imekuwa ikitushambulia kwa zaidi ya miaka 25 sasa na kusababisha watu zaidi ya milioni 40 kuuawa huku Ufaransa ikinyamaza kimya bila ya kuchukua hatua. Amehoji, halafu leo Bwana Macron angependa kuja hapa kutuhurumia? Kulia machozi ya mamba?

Muandamanaji mwingine wakati huo huo alisikika akisema kuwa"tunapinga ziara ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa nchini kwetu kwa sababu anainga mkono Rwanda nchi ambayo inatuuwa usiku na mchana." 

Kiongozi huyo wa Ufaransa ambaye alianza ziara yake kwa kuelekea katikati mwa Afrika  siku ya Jumatano, anatarajiwa kuwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baadaye wiki hii. Rais wa Ufaransa atakamilisha ziara yake tarehe 5 wezi huu wa Machi kwa kuzitembelea Gabon, Angola, Jamhuri ya Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo( DRC).

Eneo la mashariki mwa Kongo limekumbwa na mapigano na machafuko kwa takriban miaka 30 sasa huku makundi mengi yenye silaha yakiendesha hujuma na mashambulizi mara kwa mara dhidi ya raia, vikosi vya serikali, na askari wa kulinda amani. Kundi la waasi la M23 ni miongoni mwa makundi hayo ambalo Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kuliunga mkono. 

Tags