Makumi ya wanaharakati wa kisiasa wauawa Kongo DR
(last modified Fri, 31 Mar 2023 02:10:58 GMT )
Mar 31, 2023 02:10 UTC
  • Makumi ya wanaharakati wa kisiasa wauawa Kongo DR

Zaidi ya wanaharakati 20 wa kisiasa wameuawa na watu wasiojulikana katika jiji la Lubumbashi, kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wanaharakati hao waliouawa katika shambulizi hilo la karibuni ni wanachama wa chama cha National Union of Congolese Federalists (UNAFEC).

Kiongozi taifa wa chama hicho, Jean Umba Lungange amesema mauaji hayo yalifanyika Ijumaa iliyopita, baada ya watu waliokuwa wamevalia magwanda wa kijeshi kushambulia kwa risasi mkusanyiko wa vijana wa chama hicho cha siasa.

Naye Bertin Tchoz, kiongozi wa shirika la kiraia linaloshughulikia masuala ya amani na usalama katika wilaya ya Haut-Katanga ambayo Lubumbashi ndiyo makao makuu yake amesema kuwa, "Makomandoo waliuawa watu 25, baadhi kwa kupigwa risasi na wengine kwa kuzamishwa (katika maji wa Mto Naviundu)."

Maeneo mengi ya mashariki ya DRC yametaliwa na harakati za uasi

Msemaji wa jeshi katika eneo hilo amesema hawana habari yoyote kuhusu mauaji hayo, na kwamba chama hicho cha kisiasa cha UNAFEC hakijaripoti tukio hilo kwa vyombo vya usalama vya nchi hiyo.

UNAFEC ambayo ni mwanachama wa jukwaa la 'Muungano Mtakatifu wa Taifa' ulioundwa na Rais Felix Tshisekedi, imekumbwa na mizozo ya ndani tangu kinara wake Gabriel Kyungu wa Kumwanza afariki dunia mwaka 2021.

 

Tags