Maporomoko ya udongo yauwa watu wasiopungua 21 mashariki mwa Kongo
(last modified Tue, 04 Apr 2023 07:07:24 GMT )
Apr 04, 2023 07:07 UTC
  • Maporomoko ya udongo yauwa watu wasiopungua 21 mashariki mwa Kongo

Watu wasiopungua 21 wamepoteza maisha na wengine kadhaa hawajulikani walipo hadi sasa siku mbili baada ya maporomoko ya udongo kutokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Miili ya wanawake 8 na watoto 13 imepatikana baada ya maporomoko ya udongo kutokea katika eneo moja la mtoni juzi Jumapili huko Bolowa wakati raia hao walipokuwa wakifua nguo na vyombo vya jikoni. Mtu mmoja amenusurika katika maafa hayo ya maporomoko ya udongo huko Bolowa. Msemaji wa Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini linalolijumuisha eneo la Masisi ameeleza kuwa jitihada za uokoaji ziliendelea kufanywa hadi jana ili kuweza kuwapata manusura.  

Naye Fabrice Muphirwa Kubuya Mkuu wa Taasisi ya Kiraia ya Osso- Banyungu amesema kuwa maporomo ya udongo yalitokea mchana wa juzi katika kijiji cha Bulwa na kwamba hadi sasa watu 30 wanaaminika kuaga dunia katika janga hilo.  

Ameongeza kuwa maporomoko ya udongo huwenda yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa mtawalia. 

 

Tags