-
Gen-Z Morocco wamlazimisha mfalme kufanya mageuzi ya kimsingi
Oct 11, 2025 02:06Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco jana Ijumaa alitoa amri ya kufanyika mageuzi ya kimsingi ili kulinda haki za kijamii wakati huu ambapo nchi hiyo imekumbwa na maandamano yanayoongozwa na vijana wanaolalamikia huduma mbovu za kijamii na ukosefu wa usawa.
-
WFP yaonya juu ya kuongezeka njaa miongoni mwa wakimbizi nchini Ethiopia
Oct 11, 2025 02:05Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) jana Ijumaa lilionya kwamba wakimbizi nchini Ethiopia wako katika hatari ya kuteseka zaidi kwa njaa huku uhaba mkubwa wa fedha ukisababisha kupunguzwa mgao wa chakula.
-
Somalia na Djibouti zakaribisha usitishaji vita Gaza; zatoa wito wa kuasisiwa taifa huru la Palestina
Oct 10, 2025 23:04Somalia na Djibouti zimekaribisha makubaliano ya amani yaliyofikiwa kwa ajili ya kusitisitisha vita katika Ukanda wa Gaza na kupongeza juhudi za kikanda na kimataifa za kufanikisha usitishaji vita, kuhahkikisha misaada ya kibinadamu inafika Gaza na wafungwa na mateka wote wanaachiwa huru.
-
Mlipuko nadra wa homa ya Bonde la Ufa wauwa watu 17 Senegal
Oct 10, 2025 23:01Mamlaka za afya nchini Senegal zimethibitisha kuaga dunia watu 17 katika kile kinachoelezwa kuwa mlipuko mkubwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF). Mlipuko huu wa homa ya Bonde la Ufa umetajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kuiathiri Senegal katika miongo kadhaa.
-
Ruto: Kuondolewa viza Afrika kutatatua changamoto za bara hilo
Oct 10, 2025 03:05Rais William Ruto wa Kenya ameahidi kuongoza juhudi za kuondoa masharti ya viza kwa Waafrika na kutatua mizozo inayokumba bara hilo.
-
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria yataka kuachiliwa wanaharakati wa Sumud
Oct 10, 2025 02:55Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imelaani kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kuendelea kuwashikilia wanaharakati wa msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Gaza, na kutaka kuachiwa mara moja kwa raia wa Nigeria na wa mataifa mengine waliotekwa nyara na kuzuiliwa na askari wa majini wa Kizayuni.
-
Tshisekedi amtaka Kagame aache kuwaunga mkono waasi
Oct 09, 2025 23:01Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amemtaka mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kuacha kuwasaidia waasi mashariki ya DRC na kutengeneza amani.
-
Eritrea yapuuzilia mbali madai ya Ethiopia ya kutaka kuanzisha vita
Oct 09, 2025 22:58Eritrea imepuuzilia mbali shutuma zilizotolewa na Ethiopia kwamba nchi hiyo inajiandaa kuanzisha vita ikisema ni ''matamshi ya uchochezi''.
-
Upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati: Hatutashiriki uchaguzi mkuu wa Desemba 28
Oct 09, 2025 07:07Upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umetangaza kuwa utasusia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Disemba ambapo Rais Faustin-Archange Touadera atawania tena urais kwa muhula wa tatu.
-
Wanaharakati wa Afrika Kusini katika msafara wa Sumud; Tulimkaripia Waziri wa Israel tukiwa kizuizini
Oct 09, 2025 03:44Wanaharakati sita wa Afrika Kusini ambao waliwekwa kizuizini huko Israel baada ya kutekwa nyara kutoka katika msafara wa kimataifa wa meli kwa jina la Global Sumud Flotilla kuelekea Gaza wamesimulia hadithi za kusikitisha kuhusu walichopitia wakiwa mikononi mwa wanajeshi wa Israel.