-
Wanamgambo wa RSF washambulia hospitali jimboni Darfur; watu 12 wameuawa, 17 kujeruhiwa
Oct 09, 2025 03:44Raia wasiopungua 12 wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika jimbo la Darfur Kaskazini.
-
Rais wa Madagascar afanya mazungumzo licha ya waandamanaji kususia
Oct 09, 2025 03:43Rais Andry Rajoelina wa Madagascar jana aliyaalika makundi na asasi kadhaa za kiraia kwa ajili ya mazungumzo katika ikuu ya Rais.
-
Ethiopia yaituhumu Eritrea kuwa inajiandaa kuanzisha vita dhidi yake
Oct 09, 2025 03:43Ethiopia imeituhumu Eritrea kuwa inajiandaa kuanzisha vita dhidi yake. Ethiopia imetoa tuhuma hizi dhidi ya Eritrea ikiwa ni ishara ya karibuni ya kushtadi mvutano katika nchi mbili hizo jirani kuhusu udhibiti wa Bahari Nyekundu.
-
ICRC: Mgogoro wa afya Kongo DR unazidi kuwa mbaya
Oct 08, 2025 23:41Mfumo wa huduma za afya katika eneo linalokumbwa na migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umezorota kwa kiasi kikubwa, huku vituo vingi vya matibabu vikiwa na uhaba mkubwa wa dawa na wafanyakazi, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imeonya katika taarifa yake ya jana Jumatano.
-
Somalia yakanusha vikali kufikia makubaliano ya siri na Sweden kuhusu kuwarejesha nchini raia wake
Oct 08, 2025 08:58Ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia leo imetoa taarifa na kukadhibisha vikali Somalia kwamba imefikia makubaliano ya siri na Sweden kuhusu kuwarejesha nyumbani raia wa Somalia kutoka Sweden ukiwemo pia mpango wa msaada wenye masharti kwa Somalia.
-
Rais wa Madagascar kufanya mazungumzo ya kitaifa leo
Oct 08, 2025 03:06Rais Andry Rajoelina wa Madagascar amesema anapanga kufanya "mazungumzo ya kitaifa" na makundi mbalimbali leo Jumatano baada ya vijana waandamanaji kutoa makataa ya saa 48 ili akubali matakwa yao la sivyo akabiliwe na maandamano ya kitaifa.
-
Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi kuhusu machafuko kaskazini mwa Msumbiji
Oct 08, 2025 03:05Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi ulionao kuhusu idadi kubwa ya raia wanaokimbia machafuko yanayoendelea kaskazini mwa Msumbiji, ambapo wengi wao wamefikia hatua ya kukata tamaa.
-
Mazungumzo ya waasi wa M23 na serikali ya Kinshasa katika hatihati
Oct 07, 2025 23:12Wakati mapigano yakiripotiwa kuendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumeibuka swali iwapo awamu ya sita ya mazunguumzo kati ya kundi waasi AFC/M23 na serikali ya Kinshasa yatafanyia juma hili jijini Doha kama ilivyotangazwa na mpatanishi nchi ya Qatar au la.
-
Vikosi vya usalama vya Kongo vyashutumiwa kwa unyanyasaji
Oct 07, 2025 06:50Tangu mapema mwezi huu wa Oktoba, kikosi cha ulinzi wa rais wa Kongo Brazzaville kimeanzisha operesheni dhidi ya magenge ya wahalifu ya vijana wanaoshambulia watu kwa mapanga wanaojulikana kwa jina maarufu la 'bebe noir' au watoto weusi.
-
Mto Nile nchini Sudan wafurika, maji ya Blue na White Nile yaongezeka
Oct 07, 2025 06:28Mafuriko makubwa katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 30 na maelfu ya wengine kukwama. Wakazi wa eneo hilo wanaelezea jinsi walivyopitisha usiku wa hofu wakati mafuriko yalipopita katikati ya nyumba na mashamba yao.