-
Serikali ya Tanzania yatakiwa itoe taarifa kuhusu aliko Polepole
Oct 07, 2025 02:39Wanaharakati na mawakili nchini Tanzania wametoa wito kwa mamlaka za usalama nchini humo kutumia rasilimali zote kuhakikisha hali ya usalama wa Balozi mstaafu Humphrey Polepole inafahamika na kuwekwa wazi kwa umma, kufuatia taarifa zinazosambaa zikidai kuwa mwanasiasa huyo ametekwa.
-
ICC yamtia hatiani kiongozi wa kwanza wa wanamgambo wa Darfur kwa uhalifu wa kivita
Oct 07, 2025 02:39Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC jana Jumatatu ilimtia hatiani kiongozi wa kwanza wa wanamgambo wa Janjaweed aliyepandishwa kizimbani akihusishwa na ukatili na jinai zilizofanyika katika jimbo la Darfur nchini Sudan zaidi ya miaka 20 iliyopita.
-
Rais wa Madagascar amteua jenerali wa jeshi kuwa Waziri Mkuu mpya
Oct 06, 2025 23:41Rais Andriy Rajoelina wa Madagascar amemteua Jenerali Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo wiki moja baada ya kulivunja baraza la mawaziri kufuatia maandamano ya wananchi ya siku kadhaa.
-
Watu 13 wameuawa na 19 kujeruhiwa katika mashambulizi ya RSF Darfur Kaskazini
Oct 06, 2025 23:41Mtandao wa Madaktari nchini Sudan leo Jumatatu umetangaza kuwa raia wasiopungua 13 wameuawa na 19 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur Kaskazini.
-
Mripuko wa boti magharibi mwa Libya waua watu kadhaa
Oct 06, 2025 23:40Watu wasiopungua watatu wamethibitishwa kuuawa katika mripuko wa boti uliotokea kwenye pwani ya Zawiya, karibu kilomita 60 magharibi mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.
-
Familia 1,200 zahama makazi yao kutokana na mafuriko Khartoum, Sudan
Oct 06, 2025 03:45Zaidi ya familia 1,200 za Sudan zimefurushwa katika nyumba zao na mafuriko katika mji wa Bahri katika jimbo la Khartoum, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilisema hayo jana Jumapili.
-
Bunge la Chad lajiunga na mkondo wa kuondoa ukomo wa mihula ya urais, lamfungulia njia Deby Itno
Oct 05, 2025 22:53Bunge la Chad limeidhinisha kwa wingi mkubwa sana wa kura marekebisho ya katiba yanayoondoa ukomo wa mihula ya urais, na kurefusha muda wa kila muhula kutoka miaka mitano hadi saba, hatua ambayo wakosoaji wanasema ni mbinu ya kuuzatiti utawala wa Rais Mahamat Idriss Deby Itno.
-
Wakfu wa Mandela walaani shambulio la Israel dhidi ya msafara wa Sumud
Oct 05, 2025 07:11Wakfu wa Nelson Mandela, taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa kwa ajili ya kumbukumbu ya rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, imelaani amelaani vikali shambulio la utawala wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Gaza, na kutaka kuachiwa mara moja kwa wanaharakati waliotekwa nyara na kuzuiliwa na askari wa majini wa Kizayuni.
-
Serikali ya Somalia yathibitisha kuuawa kwa magaidi wa Al-Shabab katika shambulio la gereza jijini Mogadishu
Oct 05, 2025 07:10Serikali ya Somalia imethibitisha kuwa wapiganaji saba wa kundi la kigaidi la Al-Shabab wanaofungamana na kundi la kigaidi la al-Qaeda wameuawa baada ya makabiliano ya saa kadhaa kufuatia shambulio kubwa dhidi ya gereza la Godka Jilow mjini Mogadishu, tukio ambalo ni miongoni mwa mashambulizi makubwa zaidi katika mji mkuu kwa miezi ya hivi karibuni.
-
Waandamanaji nchini Morocco: Tunahitaji zaidi hospitali kuliko viwanja vya soka
Oct 05, 2025 04:07Makabiliano makali yanaripotiwa kutokea baina ya waandamanaji na vyombo vya usalama nchini Morocco.