-
Kushtadi mashambulizi ya kigaidi huko Pakistan; sababu na taathira zake
Nov 04, 2023 08:12Kitengo cha Mahusiano ya Umma cha Jeshi la Pakistan kimetangaza kuwa vikosi vya jeshi hilo vimesambaratisha shambulio la kigaidi la leo asubuhi katika kambi ya kikosi cha jeshi la anga katika mji wa Mianwali katika jimbo la Punjab. Wavamizi watatu wameuwa na magaidi kadhaa wamekimbia eneo la tukio.
-
Nukta muhimu katika hotuba ya Hassan Nasrullah kuhusu Kimbunga cha al-Aqsa
Nov 04, 2023 03:36Huku akikosoa vikali katika hotuba yake ya jana Ijumaa, kimya cha nchi za Kiarabu kuhusiana na jinai zinazotekelezwa na utawala ghasibu wa Israel unaokalia kwa mabavu Quds Tukufu, dhidi ya watu wa Gaza, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, amesisitiza kuwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imetekelezwa kikamilifu na Wapalestina, kwa ajili ya taifa la Palestina na malengo yao matukufu.
-
Mpira wa kugeuzwa vita vya Ghaza kuwa vita vya kieneo uko katika uwanja wa Israeli na waungaji mkono wake wa Magharibi
Nov 03, 2023 22:56Katika siku ya 29 ya Vita vya Ghaza, maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza yakiwemo ya az-Zaitun, al-Karamah na Beit Hanoun yangali yanashambuliwa kinyama na utawala katili wa Israel.
-
Kuendelea jinai za Wazayuni dhidi ya raia wa Gaza kwa uungaji mkono wa wazi wa Marekani
Nov 03, 2023 04:45Ikiwa ni katika muendelezo wa mauaji ya raia yanayofanywa na utawala unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, ndege za kivita za utawala huo hivi karibuni zilishambulia kwa mabomu kambi ya wakimbizi ya Jabalia iliyoko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kuua kwa umati zaidi ya raia mia moja wa Palestina na kujeruhi wengine zaidi ya mia tatu.
-
Misimamo inayogongana ya White House na Biden kuhusu kusitishwa mapigano huko Ghaza
Nov 02, 2023 23:57Ikiwa zimepita takribani wiki 4 tangu kuanza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na mashambulizi ya jinai ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa maelfu ya Wapalestina hususan watoto na wanawake, Marekani ambayo ni muungaji mkono mkuu na mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni, bado inataka kuendelezwa mauaji ya umwagaji damu huko Ghaza.
-
Kuendelea siasa za undumakuwili za Erdogan kuhusu uungaji mkono kwa watu wa Gaza
Nov 02, 2023 08:18Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki anaendeleza siasa zake za undumakuwili katika kuunga mkono watu wa Ghaza, huku ndege za kivita za kistratijia za Marekani zikiwa zimeegeshwa katika kituo cha kijeshi cha Incirlik kusini mwa Uturuki.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu: "Mauti kwa Marekani" si nara tu bali ni msimamo imara
Nov 02, 2023 04:43Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika mkutano na maelfu ya wanafunzi waliotoka katika pembe zote za Iran, ameyataja matukio ya tarehe 13 Aban 1358 (November 4, 1979) kuwa pigo la Taifa la Iran kwa Marekani.
-
Kuendelea uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni; miaka 106 baada ya Azimio la Balfour
Nov 01, 2023 22:49Tarehe 2 Novemba 2023 inaambatana na maadhimisho ya miaka 106 ya Azimio maarufu la Balfour.
-
Ulimwengu unasubiri hatua ya kivitendo ya Mahakama ya Kimataifa kuhusu jinai za Gaza
Nov 01, 2023 08:06Katika kikao cha 21 cha mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachojadili ripoti za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliashiria nafasi ya mahakama hiyo na kusema: Hivi sasa tunashuhudia mauaji ya kimbari yakitekelezwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Bila shaka , jinai zinazotendeka huko Ghaza ni mfano wa wazi wa jinai za kimataifa zinazopasa kushughulikiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
-
Wasiwasi wa viongozi wa Ulaya kuhusu kuenea barani humo uungaji mkono kwa taifa la Palestina
Nov 01, 2023 02:58Kutokana na kuendelea hujuma ya kinyama inayofanywa na utawala haramu wa Isreal katika Ukanda wa Ghaza na mauaji ya umati yanayofanywa kila siku na utawala huo dhidi ya Wapalestina hususan watoto na wanawake, mwenendo wa uungaji mkono wa kimataifa kwa kadhia ya Palestina na kulaaniwa vitendo vya jinai za Israel katika ukanda huo umeongezeka, suala ambalo limewatia wasiwasi mkubwa watawala wa Ulaya.