-
Indhari ya Umoja wa Mataifa kwa wanamgambo wa Taliban
Oct 01, 2022 00:34Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Afghanistan (UNAMA) amekosoa vikali hatua ya wanamgambo wa Taliban wanaotawala nchini humo ya kutochukua hatua kuboresha haki za watu katika nchi hiyo hususan ya mabanati na wanawake na kuonya kuwa, yamkini subira ya jamii ya kimataiifa kuhusiana na utendaji wa wanamgambo hao ikafikia kikomo.
-
Mkwamo mpya wa kisiasa Lebanon baada ya Bunge kushindwa kumchagua Rais
Sep 30, 2022 09:07Kikao cha kwanza cha Bunge la Lebanon kilichoitishwa kwa ajili ya kumchagua Rais mpya wa nchi hiyo kilimalizika Alkhamisi ya jana bila ya kuwa na natija.
-
Kuimarishwa nafasi ya watoto wa Mfalme Salman katika utawala wa kiukoo wa Saudi Arabia
Sep 29, 2022 21:31Mfalme wa Saudi Arabia amemteua Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme na mwanaye, kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Pia, Mfalme Salman amemteua mwanaye mwingine, Khalid bin Salman, kuwa Waziri wa Ulinzi.
-
Undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusiana na haki za binadamu nchini Iran
Sep 29, 2022 08:27Huku Wamagharibi wakiendelea kuwachochea wananchi wa Iran kufanya ghasia na maandamano yenye uharibu, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani misimamo na mienendo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi mkabala wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na haki za binadamu.
-
Ukosoaji wa China kwa vikwazo vya Marekani vinavyosababisha masaibu kwa nusu ya watu wote duniani
Sep 28, 2022 22:56Wizara ya Mambo ya Nje ya China imeikosoa Marekani kwa kutekeleza sera ya vikwazo na kusababisha matatizo na masaibu kwa nusu ya watu wote duniani.
-
Usitishaji usiositishwa wa vita vya Yemen
Sep 28, 2022 05:32Sambamba na kukaribia tarehe Pili Oktoba, siku utakapokamilika muhula wa miezi miwili wa usitishaji vita nchini Yemen, zoezi la kusimamisha mapigano katika vita vya nchi hiyo ambalo lilianza rasmi tarehe Pili Juni mwaka huu, litakuwa limekamilisha duru yake ya pili.
-
Kubadilishwa ghafla faili la kesi ya Mahsa Amini kuwa mradi wa mapinduzi dhidi ya serikali
Sep 27, 2022 22:48Kwa kuzingatia kuwa utawala haramu wa Israel uliamuru hadharani kuuawa kigaidi Shirin Abu Akleh, mwandishi wa habari wa Kipalestina wa televisheni ya al-Jazeera, Mkristo ambaye pia alikuwa na uraia wa Marekani akiwa kazini huko Jenin, na ambapo umeshindwa kuhalalisha kitendo hicho, hivyo umeamua kukaa kimya kwa sasa kuhusu kifo cha Mahsa Amini.
-
Mkusanyiko wa mamilioni ya watu wa Iran; kufukuzwa wafanyaghasia na Umma wa Mtume Mtukufu (saw)
Sep 27, 2022 04:11Wananchi wa mikoa tofauti ya Iran siku ya Jumapili, ambayo ilisadifiana na siku ya kukumbuka kifo cha Mtukufu Mtume (saw) na mkuu wake Imam Hassan Mujtaba (as), walifanya mkusanyiko wa mamilioni ya Umma wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambapo walilaani vikali machafuko ya hivi karibuni nchini na pia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.
-
Kuongezeka maradufu bajeti ya kijeshi ya UK, kushiriki London kwenye chokochoko za kijeshi za Washington
Sep 26, 2022 22:42Licha ya Uingereza kukumbwa na mgogoro wa kiuchumi baada ya janga la corona na kupungua thamani ya sarafu ya nchi hiyo, lakini London imeamua kuongeza maradufu bajeti yake ya matumizi makubwa ya kijeshi.
-
Kombora jipya la Korea Kaskazini na kiwingu kizito cha vita Kusini Mashariki mwa Asia
Sep 26, 2022 04:50Hatua ya Korea Kaskazini ya kufanyia majaribio kombora lake jipya kuelekea upande wa Bahari ya Japan imepokewa kwa hisia kali na nchi mbili za Japan na Korea Kusini.