-
Shutuma na bwabwaja za uwongo za Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran
Mar 08, 2025 07:17Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani haiwezi kuangamizwa kwa shambulio la kijeshi. Araqchi ameeleza haya akijibu uropokaji na uwongo wa Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya nchi hii.
-
Trump na kukandamizwa uhuru wa kusema huko Marekani
Mar 08, 2025 00:53Gazeti la Marekani la Washington Post limeandika makala likiashiria amri za utendaji zilizotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, tangu aingie madarakani na kusema: Wakosoaji wanamtuhumu kuwa anakandamiza sana uhuru wa kujieleza na kukiuka Katiba ya Marekani.
-
Kwa nini Rwanda imeitaka Uingereza iilipe fidia?
Mar 07, 2025 07:04Suala la madai ya Rwanda ya fidia ya pauni milioni 50 kutoka kwa Uingereza kwa kuacha mpango wa kuwafukuza wakimbizi haramu nchini humo sasa limekuwa kadhia tata na ngumu kati ya nchi hizo mbili.
-
Onyo la Iran kwa Troika ya Ulaya kwa kukiuka Azimio la Umoja wa Mataifa na JCPOA
Mar 06, 2025 23:01Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa yaliyoko mjini Vienna, ametoa indhari kwa Troika ya Ulaya kuhusiana na ukiukaji wake wa Azimio la Umoja wa Mataifa na la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA.
-
Mpango wa Ulaya wa kujibu mapigo kwa hatua ya upande mmoja ya Trump kuhusiana na vita vya Ukraine
Mar 06, 2025 03:53Viongozi wa nchi za Ulaya wameamua kuchukua hatua zaidi za kuandaa mkakati wa kuwa na mpango huru na wa kujitegemea kiulinzi kufuatia msimamo na uamuzi wa upande mmoja uliochukuliwa na Marekani kuhusiana na vita vya Ukraine.
-
Kwa nini Iran inakaribisha upanuzi wa ushirikiano na Afghanistan?
Mar 05, 2025 22:56Majadiliano na mikutano ya maafisa wa Iran na Afghanistan yanaendelea kwa lengo la kupanua uhusiano na kutatua masuala kati ya nchi hizi mbili.
-
Mpango wa Umoja wa Nchi za Kiarabu kuhusu Palestina unapingana na matakwa ya Marekani na Utawala wa Kizayuni
Mar 05, 2025 04:43Viongozi wa nchi za Kiarabu, katika mkutano wao mjini Cairo, wamepinga mipango na njama za kishetani za Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kukataa hatua za kulazimisha uhamishaji wa Wapalestina.
-
Mkutano wa London, maonyesho ya nguvu na uungaji mkono kwa Ukraine bila dhamana ya utekelezaji
Mar 05, 2025 00:46Siku mbili baada ya kufedheheshwa Rais Zelensky wa Ukraine katika Ikulu ya White House na suala hilo kuakisiwa pakubwa kimataifa, viongozi wa nchi 19 za Ulaya, Canada na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya na muungano wa NATO wamekutana mjini London kwa ajili ya kutangaza mshikamano wao na Ukraine katika vita vyake na Russia.
-
Uvurugaji wa utawala wa Kizayuni na kuongezeka wasiwasi kuhusu kuvunjika usitishaji vita huko Ghaza
Mar 04, 2025 07:47Huku awamu ya kwanza ya usitishaji vita na kubadilishana wafungwa na mateka kati ya utawala wa Kizayuni na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas), ikiwa imemalizika, baraza la mawaziri la Netanyahu limeongeza wasiwasi wa kuanzishwa tena vita dhidi ya Ukanda wa Gaza, kwa kuvuruga mazungumzo ya utekelezaji wa awamu ya pili ya usitishaji vita.
-
Misaada ya kijeshi na silaha ambayo haijawahi kutolewa mfano wake ya serikali ya Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Mar 03, 2025 23:28Sambamba na Marekani kukata misaada yake kwa Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, siku ya Jumapili alitumia mamlaka ya dharura aliyonayo kisheria kupitisha mpango wa utoaji msaada wa shehena ya silaha zenye thamani ya dola bilioni 4 kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.