Jerusalem Post: Wayemen hawawezi kushindwa
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i130106-jerusalem_post_wayemen_hawawezi_kushindwa
Katika ripoti yake ya siku ya Jumatano, gazeti moja la Kizayuni sambamba na kusisitiza kutoweza kushindwa taifa la Yemen limesema kuwa, utawala ghasibu wa Israel hautaki kuingia katika mzozo wa moja kwa moja na Yemen.
(last modified 2025-08-28T08:09:49+00:00 )
Aug 28, 2025 08:08 UTC
  • Jerusalem Post: Wayemen hawawezi kushindwa

Katika ripoti yake ya siku ya Jumatano, gazeti moja la Kizayuni sambamba na kusisitiza kutoweza kushindwa taifa la Yemen limesema kuwa, utawala ghasibu wa Israel hautaki kuingia katika mzozo wa moja kwa moja na Yemen.

Katika ripoti yake hiyo, gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post limesisitiza kuwa, tangu Oktoba 2023 utawala wa Israel umeshindwa kuwazuia Wayemen kurusha makombora na ndege zisizo na rubani na kuongeza kuwa: 'Israel haijataka kuwa na mzozo wa moja kwa moja na Yemen tangu mwanzo na imejaribu kuiachia Marekani suala hili.' Jerusalem Post, likiwanukuu maafisa wa ngazi za juu wa Kizayuni, limeandika: 'Wayemen ni wendawazimu kuliko pande zote katika eneo hili na kupigana nao ni kubaya sana kwa Israel kwa sababu hawawezi kushindwa.' Gazeti hili la Kizayuni limeongeza kuwa: 'Maafisa wa Marekani wamethibitisha madai ya maafisa wa Israel kuhusu kutoshindwa kwa Wayemen.' Jerusalem Post limeandika: 'Serikali ya Israel ilitangaza hadharani na kwa fahari kwamba Sana'a ingebaki bila umeme kwa muda mrefu, lakini katika kipindi kifupi, Wayemen wote waliunganisha umeme na wakati huo huo kurusha kombora jipya dhidi ya Israel.' Gazeti hilo la Kizayuni pia limeikosoa serikali ya Marekani kwa kuandika: 'Uamuzi wa utawala wa Donald Trump wa kusimamisha mgogoro na Yemen umeiacha Israel peke yake mbele ya dhoruba.'