-
Hali ya utulivu yarejea Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya mapigano + Sauti
Dec 27, 2019 12:18Hali ya utulivu imerejea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui baada ya siku mbili za mapigano baina ya makundi mawili hasimu. Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu 30 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Mossi Mwasi na maelezo zaidi…
-
Uganda yapongezwa na WHO kwa kukazania afya ya jamii + Sauti
Dec 27, 2019 12:15Serikali ya Uganda imepongezwa kwa kusimamia na kukazania vyema afya katika jamii kuanzia mashinani. Pongezi hizo zimetolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala…
-
Waziri wa zamani wa DRC ataka Rwanda ivamiwe na kugeuzwa mkoa ili mashariki mwa DRC kuwe salama + Sauti
Dec 25, 2019 07:14Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Adolphe Muzito amesema kuwa, njia pekee ya kumaliza uasi mashariki mwa nchi hiyo ni kuivamia nchi jirani ya Rwanda na kuigeuza kuwa mkoa wa DRC. Mossi Mwasi na maelezo zaidi.
-
Mashinikizo ya wananchi yailazimisha serikali DRC kufuta sherehe za kukabidhiwa madaraka Tshisekedi + Sauti
Dec 23, 2019 06:29Serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imelazimika kufutilia mbali sherehe za kupokezana madaraka kwa njia ya amani baina ya rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila na rais wa hivi sasa Felix Tshisekedi. Hii in baada ya wananchi na asasi za kiraia kulalamikia gharama kubwa za hafla hizo zilizotazamiwa kufanyika tarehe 24 Januari mwakani. Mwandishi wetu Mossi mwazi na maelezo zaidi.
-
SAUTI, Hatimaye Francois Bozize rais wa zamani wa CAR arejea nchini humo kwa uficho
Dec 17, 2019 12:29Aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize amerejea nchini humo katika hali ya uficho.
-
Mkuu wa Mkoa wa Tabora afuta mapumziko ya Mwaka Mpya; watu wakalime pamba + Sauti
Dec 15, 2019 12:50Nchini Tanzania, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza kuakhirishwa likizo ya A-Mass na mwaka mpya kwa maafisa wa kilimo na maafisa wote katika kipindi hiki cha mvua, ili watoke waende vijijini wakawahimize wananchi kulima pamba kwa ubora unaotakiwa. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam, Tanzania
-
SAUTI, Mkatasa wa kukwama mazungumzo kati ya Rwanda na Uganda, licha ya nchi kadhaa kujitahidi kufanya upatanishi
Dec 14, 2019 13:04Mazungumzo kati ya wajumbe wa Rwanda na Uganda yaliyofanyika jana Ijumaa nchini Uganda yalimalizika bila kufikiwa natija iliyokuwa ikitarajiwa.
-
SAUTI, Wapinzani Gabon: Operesheni za Rais Bongo za kupambana na ufisadi ni njama za kuwaingiza madarakani ndugu zake
Dec 13, 2019 13:10Operesheni ya Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon ya kuwatimua viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, imekumbwa na changamoto kali baada ya rais huyo kunyoshewa kidole cha lawama kwamba anazitumia operesheni hizo kwa lengo la kuwaingia madarakani watu wake wa karibu.
-
SAUTI, Usikose kutegea sikio ripoti ya matukio ya Kiislamu, kuanzia Tanzania hadi nchini Kenya
Dec 13, 2019 13:09Ripoti hii ya matukio ya Kiislamu imesheheni habari za Ijtimai iliyofanyika visiwani Zanzibar, ukaguzi wa msikiti mkubwa zaidi eneo la jangwa la sahara unaojengwa na Mfalme wa Sita wa Morocco nchini Tanzania, safari ya Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi nchini Morocco kuhudhuria kongamano la Kiislamu na hadi mjini Nyeri nchini Kenya.
-
Zarif azijibu nchi tatu za Ulaya "zilizoishitaki" Iran kwa Umoja wa Mataifa + Video
Dec 05, 2019 23:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa madai yaliyotolewa na nchi tatu za Ulaya katika barua yao kwa Umoja wa Mataifa dhidi ya uwezo wa makombora wa Iran ni ya uongo na lengo lake ni kuficha kushindwa nchi hizo kuheshimu angalau kidogo ahadi zao katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA.