Islami: Iran iko tayari kuuza bidhaa zinazotokana na maji mazito ya nyuklia
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ametangaza utayarifu wa kuuza nje bidhaa zinazotokana na maji mazito za Iran.
Mohammad Eslami ameashiria mafanikio ya shirika hilo katika sekta ya leza na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa katika sekta ya ubunifu wa leza kutokana na bioteknolojia kwa msaada wa maji mazito ambayo yanatumika katika dawa za deuterium.
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameeleza kuwa: Mazao ya maji mazito ni mojawapo ya mafaniko ya karibuni katika nchi zilizoendelea na ni nchi mbili au tatu tu zinazojishughulisha katika uwanja huo.
Teknolojia ya nyuklia ni kati ya teknolojia muhimu na za msingi iliyo na nafasi kubwa katika kukuza teknolojia nyingine mpya na maendeleo ya viwanda vya kisasa.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia inategemea uwezo wa wataalamu wake wa ndani na kustafidi na nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani, na imethibitisha kwa nia njema kwamba, haina lengo zaidi ya matumizi ya amani na viwanda ya nishati hii.