Kan'ani ayakosoa mataifa yanayounga mkono ugaidi ili kuvuruga usalama nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101016-kan'ani_ayakosoa_mataifa_yanayounga_mkono_ugaidi_ili_kuvuruga_usalama_nchini_syria
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulio la genge la kigaidi la Daesh dhidi ya jeshi la Syria katika mkoa wa Deir ez-Zur wa mashariki mwa nchi hiyo na kukosoa vikali mataifa yanayounga mkono ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 13, 2023 09:49 UTC
  • Kan'ani ayakosoa mataifa yanayounga mkono ugaidi ili kuvuruga usalama nchini Syria

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulio la genge la kigaidi la Daesh dhidi ya jeshi la Syria katika mkoa wa Deir ez-Zur wa mashariki mwa nchi hiyo na kukosoa vikali mataifa yanayounga mkono ugaidi.

Nasser Kan'ani ameeleza kuwa, himaya na uungaji mkono kwa ugaidi nchini Syria unafanyika kwa shabaha ya kuzuia kupatikana amani na uthabiti katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa, mwenendo wa kuongezeka mashambulio ya kigaidi nchini Syria katika miezi ya hivi karibuni chimbuko lake ni kuendelea kuungwa mkono magaidi walioko Syria na lengo hasa ni kuzuia nchi hiyo kurejea katika mkondo wa amani na uthabiti kamili.

Ijumaa iliyopita, magaidi wa Daesh walilivizia basi moja lililokuwa limebeba makuruta wa jeshi la Syria na kulishambulia katika eneo la jangwani la mkoa wa Deir ez-Zur ambapo kwa akali askari 20 wa Syria waliuawa na wengine wasiopungua 0 kujeruhiwa.

 

Baada ya tukio hilo, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria ilitangaza kuwa, vikosi vamizi vya Marekani vimefanya jinai mpya kwa kushambulia basi lililokuwa limebeba askari wa jeshi la Syria kusini-mashariki mwa Deir ez-Zur, vikishirikiana na makundi ya kigaidi na kuua askari kadhaa. 

Serikali ya Syria imekuwa ikisisitiza mara kwa mara juu ya azma yake kupambana na magaidi ili kuangamiza mabaki ya makundi hayo na kwamba, itaendeleza jitihada za kukomboa ardhi yake kutoka kwenye uvamizi Marekani, utawala haramu wa Israeli na Uturuki kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Majeshi ya Marekani yanakalia kwa mabavu maeneo yenye utajiri wa mafuta ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Syria kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh.