Aug 14, 2023 13:57 UTC

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Kuwashambulia mazuwari wasio na hatia katika haram ya Ahlul Bayt ni kitendo cha kijinai.

Matamshi haya imetolewa baada ya gaidi wa kitakfiri kuingia kwenye eneo la kaburi la mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Hazrat Ahmad bin Musa (as) katika mji wa Shiraz, katika mkoa wa Fars, kusini mwa Iran, akiwa na bunduki na kuanza kuwafyatulia risasi watumishi na Waislamu walikwenda kuzuru eneo hilo tukufu.

Hadi sasa, mtu mmoja ameripotiwa kuuliuawa shahidi katika tukio hilo la kigaidi na wengine wanane wamejeruhiwa. Gaidi aliyehusika wa shambulizi hilo alikamatwa na maafisa wa usalama na polisi waliofika kwa wakati.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani Chafi, amelaani shambulio la kigaidi katika haram ya Sayyid Ahmad Bin Musa (as) huko Shiraz na kusema: "Baadhi ya madola yanatumia makundi ya kigaidi na kitakfiri, wakiwemo magaidi wa ISIS kwa ajili ya kupenya na kuingia katika eneo hili la Magharibi mwa Asia.

Haram ya Sayyid Ahmad bin Musa, Shiraz

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa: Magaidi wahalifu wanataka kulipiza kisasi cha vipigo vizito vya Jamhuri ya Kiislamu na wapiganaji shupavu wa Iran dhidi ya mti habithi wa ugaidi katika miaka iliyopita kwa kuwalenga wanaume, wanawake na raia wa Iran ya Kiislamu. 

Kuhusu makubaliano ya hivi karibuni kati ya Iran na Marekani ya kubadilishana wafungwa baina ya nchi hizo mbili na vilevile kuachiliwa fedha zilizozuiwa za Iran, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Iran imepokea dhamana zinazohitajika kutoka kwa Wamarekani kwa ajili ya kutekeleza makubaliano hayo.

Nasser Kan'ani amesema kuhusu safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Saudi Arabia kwamba: Mwaliko wa Mfalme wa Saudi Arabia kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umewasilishwa rasmi lakini tarehe ya ziara hiyo bado haijaainishwa.

Tags