Iran yaanza kutengeneza satelaiti yake 'ya kisasa zaidi'
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101208-iran_yaanza_kutengeneza_satelaiti_yake_'ya_kisasa_zaidi'
Shirika la Anga za Juu la Iran (ISA) limetangaza kuzindua mchakato wa uzalishaji wa "Pars-3," satelaiti "ya kisasa zaidi na yenye usahihi wa juu sahihi"
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 18, 2023 08:47 UTC
  • Iran yaanza kutengeneza satelaiti yake 'ya kisasa zaidi'

Shirika la Anga za Juu la Iran (ISA) limetangaza kuzindua mchakato wa uzalishaji wa "Pars-3," satelaiti "ya kisasa zaidi na yenye usahihi wa juu sahihi"

Hassan Salarieh, mkuu wa shirika hilo,  amenukuliwa na tovuti ya Tasnim akisema," Hapo awali, tulitoa ahadi kadhaa kuhusu utengenezaji wa satelaiti za uchunguzi kutoka mbali zenye usahihi wa hali ya juu."

Ameongeza kuwa: "Leo, ninatangaza kwa fahari kwamba Shirika la Anga za Juu la Iran limechukua hatua muhimu sana katika kubuni na kutengeneza satelaiti za kufanya uchunguzi kwa usahihi mzuri sana."

Alizitaja "Pars-2" na "Pars-3" kama satelaiti mbili kama hizo, ambazo taratibu zake za uzalishaji "zimeanza rasmi."

Salarieh amedokeza kuwa litambua "Pars-2" na "Pars-3" kama satelaiti zenye usahihi wa upigaji picha wa mita nne na mbili.

Iran hivi sasa ni miongoni mwa nchi 10 za dunia zenye uwezo mkubwa katika anga za juu, mafanikio ambayo yamepatikana kutokana na juhudi za zaidi ya miongo 4 za wataalamu wa humu nchini, na kwa hivyo Iran ina nafasi muhimu katika sekta hii kati ya nchi chache zilizo na teknolojia hiyo. Hivi sasa, ujenzi wa vituo vya kurushia satelaiti uko mikononi mwa nchi 6 tu, na Iran iko kwenye nafasi inayofuata katika uwanja huo wa kustawisha vituo vya anga za mbali.

Iran ilirusha katika anga za mbali satalaiti yake ya kwanza kabisa inayojulikana kwa jina la Omid (yaani Tumaini) mwaka 2009.

Iran pia imetangaza kuwa, katika kipindi cha miaka michache ijayo itatuma mwanaadamu katika anga za mbali. Tayari mazoezi yameshafanyika kuhusiana na lengo hilo kwa kutumwa nyani hai katika anga za mbali ambaye alirejea ardhini akiwa salama.