Dkt. Velayati: Iran itaendelea kuunga mkono wananchi wa Palestina
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea na msimamo wake thabiti wa kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.
Dkt. Ali Akbar Velayati amesema hayo katika mazungumzo yakke kwa njia ya simu na Ismail Hania, Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu yay Palestina HAMAS na kusisitiza kwamba, Iran itaendelea pia kuunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina mkabala na Wazayuni maghasibu.
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria kukwama katikak kinamasi cha mgogoro utawala ghasibu wa Israel na kusisitiza kwamba, msimamo wa Iran wa kuwaunga mkono wananchi wa Palestina mpaka wapatiwe haki zao zilizoghusubiwa haubadiliki.
Dkt. Velayati amesifu na kupongeza pia muqawana na kusimama kidete taifa la Palestina hususan katika Ukingo wa Magharibi na kueleza kwamba, huo ni ushindi wa azma na irada ya taifa na muqawama wa wananchi wa Palestina.
Kwa upande wake Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameipongeza misimamo thabiti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwaunga mkono Wapalestina pamoja na muqawama wao dhidi ya utawala haramu wa Israel.
Ismail Hania amesema pia kuwa, hatua ya Israel ya kushadidisha jinai zake inalenga kusambaratisha azma na irada ya wananchi wa Palestina lakini adui anapaswa kutambua kwamba, muqawama wa Palestina utaendelea na njia yake na hautarudi nyuma wala kulegeza kamba mpaka utakapofikia malengo yake ikiwa ni pamoja na ni kusambaratisha mipango ya adui na kuzikomboa ardhi zote za Palestina.