Iran yafanikiwa kuzalisha Cesium-137 radionuclide inayotumika katika viwanda vya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101556-iran_yafanikiwa_kuzalisha_cesium_137_radionuclide_inayotumika_katika_viwanda_vya_nyuklia
Wataalamu wa nyuklia wa Iran kwa mara ya kwanza wameweza kuzalisha mada ya Cesium-137 radionuclide ambayo ilikuwa inaagizwa kutoka nje.
(last modified 2026-05-24T07:36:41+00:00 )
Aug 28, 2023 01:15 UTC
  • Iran yafanikiwa kuzalisha Cesium-137 radionuclide inayotumika katika viwanda vya nyuklia

Wataalamu wa nyuklia wa Iran kwa mara ya kwanza wameweza kuzalisha mada ya Cesium-137 radionuclide ambayo ilikuwa inaagizwa kutoka nje.

Mada hiyo ambayo hutumika kwa madhumuni mengi ya matibabu na viwanda ilizinduliwa wakati wa maonyesho Jumapili katika mji mkuu wa Iran, Tehran katika kikao kilichohudhuriwa na Mohammad Eslami, mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI).

Radionuclides (au radioisotopi) ni anuai atomiki za mionzi ambazo aghalabu huibuliwa katika mkondo wa nyutroni kwenye kinu cha nyuklia.

Mada hii inatumika katika vifaa vya mionzi, brachytherapy, radiotherapy, chemchemi za calibration, na aina mbalimbali za vipimo vya viwanda.

Mada hii aidha hutumika katika kutengeneza bidhaa za damu, vipodozi, chakula, na bidhaa zingine.

Katika miaka ya hivi karibuni, Iran imepata maendeleo ya ajabu katika sekta ya nyuklia licha ya vitisho na vikwazo vya madola ya Magharibi. Tehran daima imekuwa ikisisitiza kwamba mpango wake wa nyuklia unatekelezwa kwa malengo ya aman . u

Mohammad Eslami, mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI).

Akizungumza katika sherehe za Jumapili, Eslami amesema kuwa pamoja na mzunguko wa nishati ya nyuklia, Iran ina uwezo wa kubuni, kujenga na kudumisha vinu vya nyuklia, akibainisha kuwa sekta ya nyuklia ya nchi ina jukumu la moja kwa moja katika maisha ya watu.

Hali kadhalika amesema adui zetu walikuwa na wangali wanapinga sekta ya nyuklia ya Iran, lakini wote wanapaswa kujua kwamba sekta ya nyuklia ni sekta ya kimkakati.

Mkuu huyo wa nyuklia wa Iran pia amesifu utengenezaji wa Cesium-137 radionuclide kama mafanikio muhimu ya nyuklia ambayo yanaondoa utegemezi wa nchi kwa nchi zingine kwa uagizaji wa mada hiyo.

Amesema Cesium-137 radionuclide inaweza kutumika katika mifumo ya vifaa vya viwandani, maeneo ya mafuta na gesi na sekta nyinginezo.

Eslami ameongeza kwamba Iran inaendelea kushirikiana na Wakala wa Umoja wa Mataifa wa Nishati ya Atomiki na kwamba maeneo manne ya mvutano na wakala huo yamepunguzwa hadi maudhui mbili tu.