Amir-Abdollahian: Matembezi ya Arubaini ni nembo ya kupambana na dhulma
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101610-amir_abdollahian_matembezi_ya_arubaini_ni_nembo_ya_kupambana_na_dhulma
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: matembezi ya Arubaini ni nembo ya kupambana na dhulma, wito wa kukomboka na kielelezo cha mapambano yasiyo na kikomo ya kuithibitisha haki na uadilifu duniani.
(last modified 2026-07-28T12:43:49+00:00 )
Aug 29, 2023 04:19 UTC
  • Amir-Abdollahian: Matembezi ya Arubaini ni nembo ya kupambana na dhulma

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: matembezi ya Arubaini ni nembo ya kupambana na dhulma, wito wa kukomboka na kielelezo cha mapambano yasiyo na kikomo ya kuithibitisha haki na uadilifu duniani.

Hossein Amir-Abdollahian ameeleza hayo katika ujumbe wake uliochapishwa katika magazeti ya Az-Zuwaar na As-Sabah ya Iraq, na akaongeza kuwa: matembezi ya Arubaini kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa zaidi ya jamii ya wanadamu ulimwenguni, na harakati kubwa, adhimu, na yenye chimbuko na asili ambapo kila mwaka mamilioni ya Waislamu kutoka kila pembe ya ulimwengu wa mataifa, rangi na lugha tofauti hukusanyika pamoja.

Waziri Hossein Amir-Abdollahian

Amir-Abdollahian amesema, imani juu ya dini, kumtegemea Mwenyezi Mungu, maadili, uadilifu, kutetea wanyonge na wanaodhulumiwa duniani, kukaribiana nchi za Kiislamu, kukabiliana na mfumo wa ubeberu na kuthibiti fikra ya umma mmoja wa Kiislamu, ambayo ni moja ya vielezi vya ustaarabu wa kisasa wa Kiislamu, ni miongoni mwa nukta za msingi za Matembezi ya Arubaini.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyaelezea Matembezi ya Arubaini kuwa ni mfano pia wa mafanikio ya sera ya ujirani mwema baina ya nchi mbili za Iran na Iraq.../