Amir-Abdollahian: Askari wa Marekani ondokeni Asia Magharibi; rudini mlikotoka
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101678-amir_abdollahian_askari_wa_marekani_ondokeni_asia_magharibi_rudini_mlikotoka
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewashauri wanajeshi wa Marekani kurejea nyumbani na viongozi wa dola hilo la kibeberu kuwaachia watu wa Asia Magharibi eneo hilo.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Aug 31, 2023 00:20 UTC
  • Amir-Abdollahian: Askari wa Marekani ondokeni Asia Magharibi; rudini mlikotoka

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewashauri wanajeshi wa Marekani kurejea nyumbani na viongozi wa dola hilo la kibeberu kuwaachia watu wa Asia Magharibi eneo hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Hossein Amir-Abdollahian, amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Syria, Faisal al-Miqdad. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametembelea Syria akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kidiplomasia na jana Jumatano alifanya mawaziri hao wawili walifaya mazungumzo mazuri kuhusu masuala ya pande mbili, kieneo na kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amesema: Ninnapenda kulaani vikali mashambulizi ya kikatili ya utawala ghasibu wa Israel kwenye uwanja wa ndege wa Halab na maeneo ya kiraia nchini Syria. Katika eneo hili la Asia Magharibi, hakuna vitendo vya uchokozi na jinai vya utawala wa Kizayuni ambavyo havijapatiwa majibu na hakuna jinai yoyote ya Wazayuni itakayoachwa ipite vivi hivi.

Wanajeshi wa Marekani wakiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi SEPAHH baada ya kuingia kwenye maji ya Iran kinyume cha sheria

 

Amesema: Tumejadiliana pia kuhusu jinai za magenge ya kigaidi na njama za Wamarekani za kuyapanga upya magenge hayo ya kigaidi ili ipate kisingizio cha kuendelea kuwepo kibeberu nchini Syria.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: Ni wazi kwamba, usalama wa Syria na usalama wa eneo hili zima ni muhimu mno kwetu. Tutaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Syria na serikali yao ili tuweze kuwa na eneo salama, tulivu na lenye maendeleo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Amir-Abdollahian ameongeza kuwa: Tunaamini kwamba, uhusiano wa kirafiki na ujirani mwema na wa kidugu kati ya Syria na Uturuki ni kwa maslahi ya nchi zote mbili na eneo hili zima. Tunasisitizia umuhimu wa kuheshimiwa mamlaka na umoja wa ardhi ya Syria.