Kiongozi Muadhamu: Mkisimama kidete mtafika katika kilele cha mafanikio
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101936-kiongozi_muadhamu_mkisimama_kidete_mtafika_katika_kilele_cha_mafanikio
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kumbukumbu ya maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (as) hapa mjini Tehran ambapo amewahutubu wanachuo kwa kuwaambia ya kwamba, kama mtasimama kidete basi mtafika katika kilele cha mafanikio.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Sep 06, 2023 08:50 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Mkisimama kidete mtafika katika kilele cha mafanikio

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kumbukumbu ya maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (as) hapa mjini Tehran ambapo amewahutubu wanachuo kwa kuwaambia ya kwamba, kama mtasimama kidete basi mtafika katika kilele cha mafanikio.

Sambamba na kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as), kumefanyika hafla ya maombolezo kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya kamati na vikundi vya maombolezo vya wanachuo asubuhi ya leo (Jumatano) mbele ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Akihutubia katika mkusanyiko huo, Ayatullah Khamenei, amesema, kila kikao cha maombolezo ya Imam Hussein na kutawasali kwake kunaandaa mazingira ya kuungana na nuru ya kimaanawi na mwenge wenye kuwaka Kihussein na akasisitiza kwamba: Maudhui muhimu kabisa ni kudumisha uhusiano huu na kuunganisha na njia nyoofu ambapo hilo linahitajia irada na kusimama kidete.

 

Ayatullah Khamenei amebainisha akizihutubu kamati na vikundi hivyo vya maombolezo vya wanachuo kwamba, kama mtasimama kidete mtafanikiwa kufika kileleni na hivyo kufikia katika kielele cha utawala wa dini ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kusisitiza kuwa, vijana ni chimbuko la matumaini, ameashiria mahudhurio ya hamasa  hususan vijana katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein (as) kutoka Najaf hadi Karbala huko Iraq na pia katika miji mingine ya nchi na akawaambia vijana: “Kama ambavyo mlitembea kwa uthabiti kwenye matembezi ya Arubaini, basi katika njia ya utawala wa tauhidi pia mnapaswa kuwa imara, thabiti na kutotetereka  huku mkiwa na irada na daima muishi maisha kama aliyoishi Imam Hussein na mbakie katika njia ya Imam Hussein (as).