Brigedia Jenerali Jazayeri: Haki za binadamu za Kimarekani zinatambulisha ujahili wa kisasa
Naibu Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, haki za binadamu za Kimarekani zinatambulisha ujahili wa kisasa na ambao unachukiwa na fikra za waliowengi ulimwenguni.
Brigedia Jenerali Massoud Jazayeri amebainisha kuwa, Marekani ndio mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulimwenguni.
Amesema kuwa, jinai ya kutisha ya mwaka 1988 ya Marekani ya kushambulia kwa makombora ndege ya abiria ya Iran na kuua watu wote 290 waliokuwamo katika ndege hiyo ni nembo ya kisa cha kuhuzunisha cha haki za binadamu za Marekani katika historia ya leo.
Naibu Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua ya Wamarekani ya kuingilia mambo katika maeneo mbalimbali ulimwenguni na kutuma majeshi yao katika maeneo tofauti ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Brigedia Jenerali Jazayeri amebainisha kwamba, wigo wa dhulma na jinai za Marekani ni mkubwa kiasi kwamba, haki za binadamu za Kimarekani ni sawa na kutambulisha ujahili mambo leo katika zama hizi.
Afisa huyo wa ngazi za juu katika jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema pia kwamba, taifa la Iran limekuwa likiandamwa na hatua zilizo dhidi ya haki za binadamu na Marekani kutokana na utambulisho wake wa kuchukia ubeberu na kutokubali dhulma.