May 24, 2024 16:34 UTC
  • Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mapenzi makubwa ya wananchi kwa shahidi Raisi ulikuwa ujumbe kwa dunia kwa  manufaa ya Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema amemtaja Rais shahidi wa Iran kuwa ni dhihirisho la nara za Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: Mapenzi waliyoonyesha wananchi kwake yametoa ujumbe kwa walimwengu kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo alifika nyumbani kwa shahidi Rais Sayyid Ebrahim Rais wa Iran na kusema: Kuondokewa na Raisi ni hasara kubwa na isiyoweza kufidiwa. 

Ayatullah Khamenei ameashiria kushiriki kwa wingi wananchi katika mazishi ya shahidi Rais wa Iran ambako hakukujificha machoni mwa wageni kutoka nje walioshiriki mazikoni na kusema, huo ulikuwa ni ujumbe kwa dunia kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ambayo yamedhirisha nguvu iliyokita mizizi katika jamii na taifa la Iran.  

Shahidi Rais Ebrahim Raisi 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa huduma za ikhlasi za shahidi Rais wa Iran hazikuishia katika maisha yake pekee, na kuongeza kuwa: Raisi pia alitoa huduma muhimu kwa nchi baada ya maisha yake.  

Ayatullah Khamenei ameashiria pia matamshi ya wema, upendo na kujitolea wananchi katika miji mitatu baada ya ajali na kuongeza kuwa: Mikusanyiko hiyo iliyoambatana na sala na dua za kumutakia afya njema rais imedhihirisha kushikamana kwa wananchi na mapinduzi na nara za Mapinduzi ya Kiislamu. 

Tags