Nov 24, 2023 06:26 UTC
  • Kan'ani: Usitishaji vita Gaza ni hatua ya kwanza ya kusitisha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa usitishaji vita wa muda wa kibinadamu uliofikiwa Ukanda wa Gaza ni hatua ya awali kuelekea kusitisha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni unaouwa watoto.

Nasser Kan'ani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alibainisha jana kuhusu usitishaji vita wa muda wa kibinadamu huko Gaza na kukaribisha suala hilo kuwa ni hatua ya kwanza kuelekea kukomesha kikamilifu jinai za kivita za utawala ghasibu wa Kizayuni unaouwa watoto dhidi ya raia, wakiwemo wanawake na watoto wa Kipalestina. Amesema, hatua hiyo ni natija ya matokeo ya zaidi ya siku 45 istiqama ya wananchi  wa Palestina, mapambano yao, na mapambano ya kihistoria ya wanamuqawama na ni hatua ya awali ya ushindi. 

Kan'ani amesisitiza ulazima wa kuendelezwa juhudi, ubunifu na mashauriano ya kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na pande mbalimbali za kikanda na kimataifa kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na kufanya juhudi za pamoja na nchi rafiki ili kuchukuliwa hatua za haraka kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza kikamilifu usitishaji vita na kusitisha mauaji ya halaiki yanayofanywa na utawala wa Kizayuni na kufanikisha utumaji haraka wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Gaza wasio na hatia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar jana Alhamisi alitangaza kuwa usitishaji vita wamuda utaanza kutekelezwa kuanzia leo saa moja asubuhi kwa wakati wa Palestina na kwamba aawasiliano na pande zote na wasuluhishi yamekamilika na orodha ya majina ya watu watakaoachiwa huru imekabidhiwa. 

Wakati huo huo Brigedi za Qassam tawi la kijeshi la harakati ya Hamas zimetangaza katika taarifa yao kuwa usitishaji vita wa muda unaanza kutekelezwa leo Ijumaa saa moja asubuhi kwa wakati wa Palestina. 

Brigedi za Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya Hamas

 

Tags