Mahakama ya Uswidi yamhukumu kisiasa Hamid Nouri
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i106218-mahakama_ya_uswidi_yamhukumu_kisiasa_hamid_nouri
Siku ya Jumanne, Mahakama ya Rufaa ya Uswidi, katika hatua ya kisiasa na iliyo mbali na mchakato wa kisheria, ilithibitisha hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa raia wa Iran Hamid Nouri.
(last modified 2024-05-29T07:24:47+00:00 )
Dec 20, 2023 07:34 UTC
  • Mahakama ya Uswidi yamhukumu kisiasa Hamid Nouri

Siku ya Jumanne, Mahakama ya Rufaa ya Uswidi, katika hatua ya kisiasa na iliyo mbali na mchakato wa kisheria, ilithibitisha hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa raia wa Iran Hamid Nouri.

Mnamo Novemba 9, 2019, Hamid Nouri alikamatwa na askari usalama wa nchi hiyo alipowasili Uswidi kutatua matatizo ya kifamilia ya binti yake wa kulea.

Kesi ya kukamatwa Hamid Nouri imehusishwa na utata mwingi tangu kukamatwa kwake. Ukiukaji wa kanuni za mahakama, haki za binadamu na sheria za kimataifa ni miongoni mwa masuala muhimu katika faili la kesi hiyo. Mahakama ya mwanzo iliyokuwa ikishughulikia kesi ya Nouri ilianzisha vikao vya kesi hiyo Agosti 9 2021 na baada ya kufanya vikao 92 viliyojaa utata, hatimaye Juni  mwaka 2022, mahakama hiyo ilimhukumu kifungo cha maisha jela Hamid Nouri kwa njia isiyo halali, isiyo ya haki na bila ya ushahidi wa kutosha.

Mahakama ya Rufaa ya Uswidi ilianza kusikiliza kesi ya Hamid Nouri mnamo Januari 11, 2023, na mchakato wake kumalizika Novemba iliyopita. Baada ya kukamatwa Nouri alishtakiwa na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Uswidi, kwa tuhuma za kuhusika katika matukio yanayohusiana na miaka 35 iliyopita nchini Iran, na iliyowasilishwa na wanachama wa kundi la kigaidi la Munafiqin. Hayo yanajiri licha ya kuwa, kundi hilo limewaua zaidi ya raia elfu 17 wa Iran katika operesheni mbalimbali za kigaidi tokea mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kutolewa hukumu ya mahakama

Munafiqin hao pia wameorodheshwa na nchi nyingi za dunia kuwa ni kundi la kigaidi kutokana na vitendo vyao vya kijinai na ukatili dhidi ya binadamu. Wanachukiwa na Waswidi wenyewe na hata na Wairani wanaoishi katika nchi hiyo. Kwa hivyo, kutolewa hukumu na mahakama ya Uswidi kwa mujibu wa ushahidi wa kundi lililohusika na mauaji ya halaiki na kutenda jinai za kivita, yakiwemo mauaji ya maelfu ya Wairani, hakuwezi kuhalalishwa kwa njia yoyote ile.

Tukitazama namna ya kukamatwa, kufunguliwa mashitaka na matukio yanayokuhusiana na kesi hiyo, tunaona kwamba Hamid Nouri ni mhanga wa wazi wa ukiukaji sheria; polisi kutofuata mkondo wa sheria katika mchakato wa uchunguzi, kupuuzwa ushahidi na mwendesha mashtaka kutofanya uchunguzi wa kutosha kuhusiana na kesi hiyo.

Kwa mujibu wa Haibatullah Nejandimanesh, mshauri wa kisheria wa familia ya Hamid Nouri, Nouri anashitakiwa kwa kosa la kukiuka mkondo wa kesi mahakamani, huku yeye mwenyewe akiwa ni mhanga wa mkondo huo huo. Kwa mfano, wakati wa kufanyika vikao vya mahakama ya mwanzo, kati ya vikao vyote 92 vilivyofanyika, ni vikao 7 tu ndivyo vilifanyika kwa kuhudhuria Hamid Nouri mahakamani ambapo alipewa fursa ya kujitetea.

Hamid Nouri, Mwirani aliyehukumiwa Uswidi

Hii ni katika hali ambayo, kuna masuala muhimu kuhusiana na haki za binadamu ambayo hayakuzingatiwa katika kesi ya Hamid Nouri. Kwanza, ni haki yake ya kuwasiliana na familia, ambapo kuonana ana kwa ana na familia hiyo kulisimamishwa kwa muda na mawasialino ya simu pia yakakatishwa kwa karibu mwaka mmoja. Hamid Nouri kutoruhusiwa kunufaika na nyaraka za kesi yake, kuzuiwa ushahidi wa Iran katika mahakama, kukatiwa mawasiliano Nouri na wakili wa Iran na kutishiwa mashahidi wake kukamatwa na mwendesha mashtaka wa Uswidi ni masuala mengine muhimu kuhusu kesi hiyo.

Hii ni licha ya kwamba kwa mujibu wa familia ya Nouri pamoja na kanda za sauti yake mahakamani, mtuhumiwa huyo aliteswa na kunyimwa haki zake za msingi kama vile matibabu na kustahamili mateso ya kiakili na kimwili. Ni dhahiri kwamba mchakato wa kukamatwa na kushughulikiwa kesi ya Hamid Nouri unaonyesha kuwa kesi hiyo ilikuwa kuwa ya kisiasa zaidi kuliko ya kimahakama.

Kwa kuzingatia hali hiyo Kazem Gharibabadi, Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Vyombo vya Mahakama vya Iran, ameutaja uamuzi wa mahakama hiyo kuwa usio wa kisheria, wa kimaonyesho na usiozingatia haki za binadamu wala sheria zinazokubalika kimataifa.