Kongamano la Kimataifa la Kuunga Mkono Palestina lafanyika Tehran
(last modified Sat, 23 Dec 2023 07:36:00 GMT )
Dec 23, 2023 07:36 UTC
  • Kongamano la Kimataifa la Kuunga Mkono Palestina lafanyika Tehran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Kongamano la Kimataifa la Kuunga Mkono Palestina linafanyika leo mjini Tehran kwa lengo la kuunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Nasser Kanani, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amefafanua kuhusu kikao hicho na kusema: "Mkutano huu unalenga kuimarisha uungaji mkono wa kimataifa kwa Wapalestina wanaodhulumiwa na kuimarisha mashinikizo dhidi ya utawala wa Kizayuni."

Amesema kikao hicho pia kinalenga kuushinikiza utawala wa Kizayuni usitishe mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Gaza na kuondoa kabisa mzingiro dhidi ya ukanda huo sambamba na kutumwa misaada ya kimataifa ya kibinadamu kwa watu wa Palestina.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa katika mkutano huo wa kimataifa wa siku moja, viongozi wa ngazi za juu wa serikali, shakhsia mashuhuri wa kisiasa, kidini, kielimu na vyombo vya habari kutoka zaidi ya nchi 50 wanashiriki.

Kan'ani ametathmini kufanyika mkutano huu katika fremu ya muendelezo wa juhudi za kidiplomasia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono muqawama au mapambano ya wananchi madhulumu wa Palestina na hasa Gaza na kusema: "Kusimamishwa mara moja jinai za kivita na mauaji ya kimbari ya utawala wa kibaguzi wa Kizayuni dhidi ya watu madhulumu wa Palestina ni matakwa ya watafuta haki wote duniani.

 

Tags