Mar 03, 2024 12:29 UTC
  • Kupanua uhusiano wa kitamaduni kati ya Iran na Algeria kwa msingi wa misikiti

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza utayarifu wake wa kupanua uhusiano wa kiutamaduni kati ya Iran na Algeria kwa kuzingatia misikiti kama msingi na katika mwelekeo wa kuongeza maarifa, sayansi na kujenga umoja na mafungamano katika ulimwengu wa Kiislamu.

Rais Raisi ametembelea sehemu tofauti za msikiti ambao ni mkubwa zaidi Afrika, alikofahamishwa kuhusu mchakato wa ujenzi wake.

Akizungumza msikitini hapo, Raisi ameutaja umoja na mshikamano kuwa ni miongoni mwa mahitaji muhimu zaidi ya ulimwengu wa Kiislamu hivi leo na akasema kuwa, kuunda umoja na mafungamano baina ya Umma wa Kiislamu ni moja ya kazi muhimu za misikiti na ina nafasi yenye ufanisi katika suala hili.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika kikao na Imam wa Msikiti wa Jamia wa Algeria, alitaja "kueneza mafundisho ya dini na mafundisho ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na Ahlul-Bayt (AS)", kuzingatia hali ya waumini na umakini wa kutatua shida zao" ni miongoni mwa kazi muhimu za misikiti.

Aidha ameongeza kuwa, leo hii, kupaza sauti ya Waislamu wanaodhulumiwa wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, kama suala kuu la ubinadamu, kuwe katikati sehemu ya shughuli za misikiti katika nchi za Kiislamu.

Msikiti wa Jamia wa Algeria

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameeleza kuwa, kwa bahati nzuri Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Algeria zina msimamo mmoja kuhusu suala la Palestina na kusema kwamba, iwapo misimamo hiyo hiyo ya pamoja katika kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina na kukabiliana na utawala wa Kizayuni ingekuwepo  katika ulimwengu mzima wa Kiislamu, je, Wazayuni wangethubutu kufanya wanyaofanya?

Imamu wa Masjid ya Al-Jazair (Msikiti wa Jamia wa Al Jazair) akiwasilisha ripoti ya historia ya ujenzi wa msikiti huu ameashiria njama za Wafaransa kubadilisha dini na imani za taifa la Algeria katika kipindi cha ukoloni na kusema kuwa pamoja na hayo, juhudi za taifa la Algeria bado linafuata kanuni na imani zake lilirudisha uhuru kwa nchi hii na kugeuza mahali pa shughuli za kikoloni za wakoloni kuwa Msikiti Mkuu wa Algeria.

Imamu wa Msikiti wa Al Jazair alipongeza misimamo ya kijasiri na ya kihistoria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na kadhia ya Palestina ameeleza matumaini yake kuwa nchi nyingine za Kiislamu pia zitachukua hatua katika mwelekeo huo.

 

Tags