Rais wa Iran asisitiza maendeleo katika uga wa sayansi na teknolojia
(last modified Thu, 14 Mar 2024 07:18:55 GMT )
Mar 14, 2024 07:18 UTC
  • Rais wa Iran asisitiza maendeleo katika uga wa sayansi na teknolojia

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sayansi na teknoliojia ni kati ya maeneo ambayo maadui wanayatamani ili kuirudisha nyuma Iran ya Kiislamu na akasisitiza maendeleo katika uwanja huo.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi jana alikutana na wahadhiri na wasomi na kusisitiza juu ya ulazima wa  kulinda na kuboresha kiwango cha kisayansi hapa nchini. Raisi amewashauri maprofesa na wasomi hao kutoiacha fani hiyo kirahisi wanapokabiliwa na vikwazo na matatizo, bali wapambane na kumkatisha tamaa adui na kuleta matumaini katika jamii. 

Rais Sayyid Ebrahim Raisi na kundi la wahadhiri na wasomi 

Rais Ebrahim Raisi ameongeza kuwa watu na taasisi zote zinazowajibika na masuuli wanapasa kuchukua hatua za kiubunifu na za haraka ili kuharakisha maendeleo zaidi ya Iran hususan katika uga wa sayansi. 

Wasomi waliohudhuria mkutano huo wa jana na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa wasomi wa Iran ambao wamerejea nchini katika miaka ya karibuni kutoka nchi za Magharibi ili kuendelea na shughuli zao za kisayansi na ubunifu nchini.

Tags