Wananchi wa Iran waandamana katika Siku ya Kimataifa ya Quds
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika leo katika miji na maeneo mbalimbali nchini Iran.
Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika leo kote nchini Iran katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa matembezi ya Siku ya Quds Duniani yameanza leo ikiwa ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambapo kama kawaida ya kila mwaka kote nchini Iran wananchi Waislamu walioko kwenye swaumu kwa mara nyingine tena wamepaza sauti zao na kubainisha kuchukizwa kwao na jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza.
"Siku ya Quds kutoka kimbunga cha Al-Aqsa hadi kimbunga cha Al-Ahrar" ndiyo kauli mbiu ya maandamano ya mwaka huu; na kwa kuwa wananchi madhulumu wa Palestina wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya makombora na ya kinyama ya utawala wa Kizayuni kwa miezi kadhaa sasa, mwaka huu wananchi wa Iran wamemiminika kwa wingi katika maidani na barabara mbalimbali hapa nchini kabla ya saa zilizotangazwa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds.
Katika mji mkuu wa Iran, Tehran maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yalianza kutokea katika njia 10 zilizoanishwa kuelekea Chuo Kikuu cha Tehran na kutoka katika maidani ya Ferdowsi kuelekea chuo hicho kikuu huku shughuli ya mazishi ya mashahidi wa operesheni ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni unaochukiwa iliyojiri huko Syria ikiendelea.
Kamanda Ramadan Sharif, Mkuu wa Idara ya Kuu ya Intifadha na Quds alisema juzi katika mkutano na waandishi kwamba maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yatafanyika katika maeneo zaidi ya 2,000 kote nchini na kwamba mwaka huu, kwa maana halisi Siku ya Kimataifa ya Quds ni ya kimataifa; na hii ni kutokana na ustahimilivu na weledi wa harakati ya muqawama na wananchi wa Palestina.
Brigedia Jenerali Hossein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amehutubia katika maadhimisho ya leo ya Siku ya Quds Duniani.