Apr 19, 2024 02:44 UTC
  • Ustawi wa biashara ya nje yenye mlingano chini ya uongozi wa serikali ya 13 ya Iran

Kituo cha Takwimu cha Kamisheni ya Ulaya kimetangaza kuwa Katika mwezi wa kwanza wa mwaka huu wa 2024, uagizaji wa bidhaa wa Ugiriki kutoka Iran uliongezeka mara 3 na Uholanzi mara 2, nayo mauzo ya Uhispania kwa Iran yakaongezeka kwa asilimia 62 na Italia kwa asilimia 13.

Wakati huo huo uagizaji bidhaa wa Romania kutoka Iran ulioongezeka kwa asilimia 47 na kufikia thamani ya yuro milioni 3.4, huku uagizaji wa bidhaa wa Italia kutoka Iran ukiongezeka kwa asilimia 2 na kufikia thamani ya yuro milioni 12.2.   

Uagizaji wa Romania kutoka Iran pia uliongezeka kwa 47% hadi euro milioni 3.4, na uagizaji wa Italia kwa 2% hadi euro milioni 12.2. 

Kampuni ya Eurostat ilitangaza kuwa biashara kati ya Iran na nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya katika mwezi wa kwanza mwaka huu ilifikia thamani ya yuro milioni 380. 

Katika mwezi wa kwanza wa mwaka uliopita wa 2023, nchi za Ulaya zilisafirisha bidhaa zenye thamani ya yuro milioni 344 kwa Iran. Aidha Ujerumani ilikuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Iran kati ya nchi za Ulaya mwezi Januari mwaka huu huku  ikichangia asilimia 38  ya biashara yote kati ya Iran na Umoja wa Ulaya. Katika kipindi hicho hicho, Ujerumani iliiuzia Iran bidhaa za yuro milioni 100 na yenyewe ikaagiza bidhaa za yuro milioni 19.7 kutoka Iran. 

Kuongezeka biashara kati ya Iran na nchi za Ulaya

Hii ni kusema kuwa mauzo ya Ujerumani kwa Iran hayajabadilika ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.  

Ingawa kiwango cha biashara kati ya Iran na nchi za Ulaya na Magharibi hakiwiani na uwezo na vipawa vya pande zote mbili, jambo ambalo kimsingi linalotokana na nchi za Magharibi kufungamanisha pakubwa masuala ya uchumi na biashara na mielekeo ya kisiasa, hata hivyo kulinda uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na nchi za Magharibi kunaonyesha kuwa serikali ya 13 ya nchi hii imejaribu sana kudumisha uwiano katika siasa zake za nje katika nyanja zote za kiuchumi, kibiashara na kisiasa.  

Moja ya nyenzo muhimu ambazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetumia katika uga wa sera za nje katika miaka ya hivi karibuni ni diplomasia ya uchumi. Diplomasia ya uchumi kwa maana ya kuyapa kipaumbele masuala ya uchumi katika sera za nje, inachukuliwa kuwa moja ya nyenzo muhimu katika kuendeleza malengo ya muda mrefu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Vikwazo vya upande mmoja vya Marekani na kuibuka kwa athari za kiuchumi za vikwazo nchini Iran katika miaka ya mwisho ya serikali ya 12 kumetoa msukumo kwa viongozi wa Iran kuzitilia maanani na kuzingatia pakubwa suala la diplomasia ya uchumi. Biashara ya nje ina nafasi muhimu na ya kimsingi katika kufikia ukuaji wa uchumi na maendeleo kama hatua ya kusambaratisha vikwazo na kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Iran na nchi nyingine. 

Mwelekeo wa serikali ya 13 ya Iran katika uga wa biashara ya nje umekuwa katika mkondo sahihi katika miaka kadhaa ya karibuni, ambapo ukwamishaji wowote au kupunguza vizuizi vya usafirishaji na uagizaji wa bidhaa katika kipindi hiki ima umepatiwa ufumbuzi au unashughulikiwa.  

Serikali ya 13 ya Iran 

Biashara ya nje ni moja ya nyenzo muhimu za ukuaji na maendeleo ya uchumi wa nchi. Usimamizi wa uchumi katika dunia ya leo hauwezi kufikiwa bila mabadilishano ya kibiashara na nchi za nje na kutafuta na kuchangia hisa katika soko la pamoja la nchi muhimu.  

Biashara ni moja ya vipengele vinavyobainisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi yoyote ile. Hii ni kwa sababu kila nchi inakidhi mahitaji yake ya ndani kwa kuagiza bidhaa kutoka nje; na kwa kusafirisha bidhaa za viwandani, inaimarisha nafasi yake katika masoko ya kimataifa, suala linalopelekea kuimarika uchumi wa nchi husika.  

Wakati huo huo kuongezeka kiwango cha biashara ya nje kunaonyesha kupungua utegemezi wa serikali ya Iran katika mapato ya mafuta, na kunatoa matumaini ya kustawishwa sera sahihi na misngi mikuu ya uchumi. Serikali ya 13 ya Iran imeweza kupanua uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi mbalimbali duniani kwa kuimarisha sera za kuamiliana na nchi za kigeni. Hatua hii pia imeifanya Iran izidishe kiwango cha mabadilishano yake ya kibiashara na nchi mbalimbali duniani na kutotegemea maamuzi ya Marekani na nchi za Magharibi kuhusu masuala ya uchumi wake wa ndani.  

Kuongezeka uhusiano wa kiuchumi na kupanua diplomasia ya kiuchumi, mbali na kuongeza ushawishi wa kieneo wa Iran, kunaweza kupunguza mashinikizo ya kiuchumi kwa nchi kwa kiasi kikubwa.