Apr 28, 2024 07:22 UTC
  • Makamu wa Rais wa Iran asisitiza kuendeleza uhusiano na nchi za Afrika

Makamu wa kwanza wa rais wa Iran amesema kuwa, kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika imekuwa stratijia ya Iran tangu ulipopatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.

Mohammad Mokhber amesema hayo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Constantino Chiwenga Makamu wa rais wa Zimbabwe na kueleza kwamba, nchi mbili zinapaswa kuwa kufanya miamala yao ya kiuchumi kwa kutumia sarafu zao za kitaifa, na hakuna haja ya sarafu ya nchi ya tatu, ambayo ni adui wa pamoja wa mataifa yote mawili.

Katika hali hiyo, Makamu wa kwanza wa Rais wa Iran amemwambia mwenzake wa Zimbabwe, kwamba mpango wa pamoja wa ushirikiano wa miaka 10 wa nchi hizo mbili unapaswa kuendelezwa na makubaliano yaliyotiwa saini hadi sasa yanapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo.

Mazungumzo ya Mohammad Mokhber, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran na Constantino Chiwenga Makamu wa Rais wa Zimbabwe

 

Kwa upande wake Constantino Chiwenga  Makamu wa Rais wa Zimbabwe amesema kuwa, uhusiano wa Iran na Zimbabwe umekuwa ukiimarika tangu yalipopata ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na licha ya umbali wa kijiografia baina ya nchi hizo mbili, kuna malengo mengi ya pamoja baina ya nchi hizo mbili dhidi ya mfumo wa kutawaliwa.

Afisa huyo wa ngazii za juu wa Zimbabwe amelaani shambulizi la Israel dhidi ya jengo la ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus na kusema kuwa, vikwazo vikubwa vya nchi za Magharibi vinalenga kuharibu uhuru na mamlaka ya kujiwala ya Iran na Zimbabwe, hata hivyo nchi hizi mbili zinaweza kuondosha vikwazo hivyo kwa kuzidisha uhusiano wao.

Tags