Apr 29, 2024 07:21 UTC
  • Raisi: Mkono wa chuma hauwezi kuzima harakati ya wanachuo Magharibi ya kuunga mkono Palestina

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, harakati ya wanafunzi, maprofesa na wasomi wa nchi za Magharibi za kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina ni tukio kubwa lenye muelekeo mipana ambalo haliwezi kuzimwa kwa ukandamizaji, vipigo, kamatakamata na vitendo vya utumiaji mabavu.

Seyed Ebrahim Raisi, amesema hayo katika kikao na baraza lake la mawaziirii ambapo ameutaja ukandamizaji mkubwa dhidi ya maandamano ya wanafunzi yanayopinga Uzayuni na kupigwa na kutiwa mbaroni maprofesa na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Magharibi hususan katika vyuo vikuu vya Magharibi hususan Marekani kwamba, ni ukurasa mwingine wa fedheha kwa wale wanaodai kuwa ni watetezi wa uhuru wa kusema.

Rais wa Iran amesema, hii leo kwa baraka za damu safi ya mashahidi madhulumu wa Gaza, sura ya kweli ya ustaarabu wa Magharibi imekuwa wazi zaidi na zaidi kwa watu wa dunia, na imedhihirika kuwa wanaodai uhuru wa kusema hawajaheshiimu wala kufungamana na chochote ghairi ya kudumisha ubeberu wao.

Ebrahim Raisi amesisitiza kuwa, harakati na mwamko huu dhidi ya ukatili na jinai na ubeberu havitazimwa kwa utumiaji mabavu, vipigo na kutiwa mbaroni maprofesa na wanafunzi wanaowaunga mkono wananchi madhulumu wa Ghaza.

 

Maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Kizayuni yaliyoanzia katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York nchini  Marekani, sasa yamesambaa katika vyuo vikuu vingine vya nchi hiyo vikiwemo vyuo vikuu vya Yale, New York, Harvard, Texas na Southern California.  Maandamano wa wanafunzi wa vyuo vikuu kupinga mauaji ya Israel huko Palestina pia tayari yamefika katika vyuo vikuu vya nchi nyingine za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani, Canada, Uingereza na Australia.

Tags