Jun 20, 2024 03:10 UTC
  • Maafisa usalama wa Iran na Russia wakutana Tehran katika kikao cha pamoja

Maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wametilia mkazo wajibu wa kushirikiana zaidi katika kupambana na ugaidi na uhalifu wa kitaasisi na kiserikali pamoja na kupambana na mihadarati.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, Alexander Venediktov, Naibu Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia amekuja hapa nchini Iran akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa masuala ya usalama wa nchi yake kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha pili cha kila mwaka cha Manaibu wa Makatibu wa Mabaraza ya Usalama wa Taifa ya Iran na Russia, ujumbe ambao umefanya kikao muhimu cha kiusalama na wenzao wa Jamhuri ya Kiislamu hapa Tehran.

Venediktov amesema kuwa katika kikao chao na maafisa wa Iran, wamejadiliana masuala mbalimbali yakiwemo ya ushirikiano wa kiusalama wa Iran na Russia katika kupambana na ugaidi, uhalifu wa kitaasisi na kiserikali na madawa ya kulevya kwani hayo ni katika masuala ya kiistratijia ya kikanda na kimataifa.

Ugaidi ni katika hatari kubwa zaidi za karne ya 21 na shabaha ya mashambulizi ya kigaidi ambayo yanafadhiliwa na mashirika ya kijasusi ya baadhi ya nchi, ni kudhoofisha misingi ya katiba na kutozipa utulivu serikali za nchi zisizokubali kuburuzwa na mabeberu.   

Tags