Iran, Bahrain zakubaliana kuanzisha mazungumzo ya kurejesha uhusiano wa kisiasa baina yao
(last modified Mon, 24 Jun 2024 07:16:06 GMT )
Jun 24, 2024 07:16 UTC
  • Iran, Bahrain zakubaliana kuanzisha mazungumzo ya kurejesha uhusiano wa kisiasa baina yao

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Bahrain zimetoa taarifa ya pamoja na kutangaza kuweko kwao tayari kuanza mazungumzo ya kutafuta njia za kurejesha uhusiano wao wa kisiasa na kidiplomasia.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kikao cha Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Abdullatif bin Rashid Al Zayani.

Taarifa hiyo imesema kuwa, pande hizo mbili zimekubaliana kuunda mifumo muhimu ya kuanza mazungumzo kati ya nchi hizo mbili juu ya jinsi ya kuanzisha tena uhusiano wa kisiasa kati ya Tehran na Manama.

Iran, Bahrain zakubali kuanza mazungumzo juu ya kurejesha uhusiano wa kisiasa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Abdullatif bin Rashid Al Zayani anazuru mji mkuu wa Iran wa Tehran kushiriki katika mkutano wa Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia (ACD).

Zaidi ya wajumbe 30 wakiwemo mawaziri wa mambo ya nje na manaibu waziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa (ACD) watashiriki katika mkutano huo utakaoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.