Greenland; kulegeza msimamo Trump au kubadilisha mbinu?
https://parstoday.ir/sw/news/world-i135890-greenland_kulegeza_msimamo_trump_au_kubadilisha_mbinu
Vyanzo vya habari, vikiwanukuu maafisa wa NATO na Rais wa Marekani Donald Trump, vimeripoti kuanza mazungumzo kati ya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO, Marekani na Denmark kuhusu kisiwa cha Greenland pambizoni mwa mkutano wa Davos.
(last modified 2026-01-26T02:34:44+00:00 )
Jan 26, 2026 02:34 UTC
  • Greenland; kulegeza msimamo Trump au kubadilisha mbinu?

Vyanzo vya habari, vikiwanukuu maafisa wa NATO na Rais wa Marekani Donald Trump, vimeripoti kuanza mazungumzo kati ya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO, Marekani na Denmark kuhusu kisiwa cha Greenland pambizoni mwa mkutano wa Davos.

Mazungumzo kati ya NATO, Marekani, na Denmark kuhusu Greenland yamekifanya kisiwa hiki cha kimkakati kuwa katika kilele cha duru za kisiasa na vyombo vya habari duniani, na kumekuwa na uvumi ulioenea kuhusu masharti ya makubaliano yanayowezekana kufikiwa kati ya pande hizo. Uvumi unaoonyesha mabadiliko makubwa katika usawa wa nguvu na mfumo wa utawala katika nchi ya Kaskazini. Kulingana na ripoti hizi, Marekani inaweza kupata ruhusa ya kufanya shughuli za kijeshi, ujasusi, na mafunzo huko Greenland ndani ya mfumo wa makubaliano mapya bila uratibu na serikali ya Denmark, na wakati huo huo kuweza kushiriki katika baadhi ya miradi ya maendeleo ya ndani, ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa elementi adimu za ardhi, bila kupata ruhusa ya moja kwa moja kutoka Copenhagen. Kama hilo litaafikiwa itaamaanisha upanuzi usio wa kawaida wa wigo wa ushawishi wa uendeshaji wa Marekani katika eneo hilo lililojitegemea.

Katika kujibu uvumi huo, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alichukua msimamo wa tahadhari lakini wa wazi, akisema: "Tunaweza kujadili kila kitu, lakini hatutajadili uhuru wetu." Alisisitiza kwamba Denmark ilikuwa tayari kwa majadiliano "yenye kujenga" kuhusu kuongeza usalama katika Nchi ya Kaskazini, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kupelekwa mfumo wa ulinzi wa makombora wa Marekani unaojulikana kama "Golden Dome," mradi mchakato huu uambatane na kuheshimiwa kikamilifu umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala Denmark.

Kwa upande mwingine, Trump alionyesha matumaini zaidi, akiandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social: "Kulingana na mkutano wenye tija sana niliokuwa nao na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte, tumeunda mfumo wa makubaliano ya baadaye kuhusu Greenland, na kimsingi eneo lote la Nchi ya Kaskazini." Aliongeza kuwa makubaliano hayo, yakikamilika, yatakuwa "suluhisho zuri" kwa Marekani na wanachama wote wa NATO. Matamshi haya yanaonyesha kwamba makubaliano ya kati ya Trump na Katibu Mkuu wa NATO yanapaswa kuonekana kama hatua ya kianzio katika mzozo ambao umebadilika katika miezi iliyopita kutoka dai lenye utata la "kupora" kisiwa kikubwa zaidi duniani hadi makubaliano tata ya kijiografia ya matabaka kadhaa.

 

Makubaliano haya yanaonekana kuwa ni kurudi nyuma na kulegeza msimamo kutoka katika vitisho vya awali vya Trump vya kuiunganisha Greenland moja kwa moja, au yanabainisha mabadiliko ya kimkakati katika mwelekeo wa kufikia malengo yaleyale ya kimkakati ambayo utawala wake umekuwa ukifuatilia tangu mwanzo, malengo ambayo yamejikita katika ushindani unaokua kati ya mataifa makubwa katika eneo la Aktiki, wasiwasi kuhusu ushawishi wa Russia na China, na hitajio la Marekani kufafanua upya usanifu wake wa ulinzi. Katika miaka ya hivi karibuni, Greenland imetambuliwa kama moja ya vikwazo katika utaratibu wa usalama wa siku zijazo katika Aktiki, haswa katika tathmini za taasisi za kifikra kama vile Baraza la Mahusiano ya Kigeni na Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa. Kwa kutawala eneo hili, Marekani itapata njia mpya za meli na rasilimali nyingi za madini adimu. Madini haya adimu ni muhimu kwa viwanda vya kijeshi na teknolojia za hali ya juu. Kwa kuongezea, eneo la kijiografia la Greenland linaifanya kuwa mahali pazuri pa kupeleka mifumo ya tahadhari ya mapema na ulinzi wa makombora. Suala ambalo lina nafasi maalum katika hesabu za Trump, haswa ndani ya mfumo wa mpango wa ulinzi wa makombora unaojulikana kama "Golden Dome."

Trump aliongeza kwa makusudi kiwango cha madai yake tangu mwanzo kwa kupendekeza wazo la kuunganisha Greenland na Marekani. Wachambuzi katika Taasisi ya Brookings wanaona hilo kama sehemu ya mfumo wa Trump wa kujadiliana, ambapo tishio la nguvu kubwa hutumika kama chombo cha kujadiliana. Kujiondoa kwake taratibu kutoka katika matamshi ya uvamizi wa nguvu kabla ya kuwa ni ishara ya kushindwa kunabainisha kupita katika awamu ya  kuangalia mambo kwa uhalisia zaidi.

Uzoefu wa kihistoria unaonyesha kwamb,a uwepo endelevu wa kijeshi wa mataifa makubwa mara nyingi husababisha ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuchumi na unaweza kudhoofisha hatua kwa hatua uhuru wa kivitendo wa wahusika wa ndani. Katika mazingiara kama haya, Denmark, huku ikidumisha uhuru wa jina tu yumkini kivitendo ikakabiliwa na vikwazo vinavyoongezeka, na Greenland yenyewe, ambao ina jamii ndogo lakini yenye mitazamo inayoongezeka ya kupigania kujitenga, inaweza kuwa uwanja mpya wa ushindani wa ushawishi. Kwa mtazamo huu, makubaliano ya Trump na Katibu Mkuu wa NATO hayapaswi kuonekana kama mwisho, bali kama hatua katika mchakato wa kuunda upya usawa wa nguvu katika eneo la Aktiki.