Iran yalaani hotuba ya Netanyahu katika Kongresi ya Marekani
(last modified Thu, 25 Jul 2024 11:20:49 GMT )
Jul 25, 2024 11:20 UTC
  • Iran yalaani hotuba ya Netanyahu katika Kongresi ya Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Benjamin Netanyahu, mtenda jinai nambari moja wa utawala bandia wa Israel, amepakatwa kwenye mikono ya waungaji mkono wake baada ya miezi 9 ya mauaji ya kimbari na mauaji ya watoto wachanga; na fedheha ndilo neno dogo linaloweza kutumiwa kueleza kashfa hiyo.

Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema haya akizungumzia hotuba iliyotolewa jana na Bemjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel katika Kongresi ya Marekani.

Ameashiria jinai za miezi 9 za mauaji ya kimbari na mauaji ya watoto wachanga zinazofanywa na Waziri Mkuu wa Israel huko Gaza, ambaye sasa amekumbatiwa na waungaji mkono wake huko Washington na kuandika kwamba: Hivi ndivyo hadaa za miongo kadhaa za ustaarabu wa Magharibi za kutaka kujidhihirisha katika sura ya kupenda utu na ubinadamu mbele ya walimwegu zinavyoyoyoma na kutoweka, na badala yake sura ya ukatili na ya kishetani ya Marekani inafichuliwa mbele ya ulimwengu mzima. 

Kan'ani ameongeza kuwa: "Kwa sasa kauli mbiu inayosikika kutoka kwa viongozi na watawala wa Marekani na nchi za Ulaya ni ya kutetea haki za binadamu, lakini haki za asili za Wapalestina zikiwemo haki ya kuishi, usalama, maji, chakula, dawa na matibabu n.k. zinakanyagwa kwa njia ya kutisha zaidi mbele ya macho ya walimwengu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi. Watoto wa Kipalestina wanachinjwa kila siku na mchinjaji wa Tel Aviv, lakini mkabala wa uhalifu huu wote, serikali ya Marekani na Congress wanamkaribisha mnyongaji huyu (Netanyahu) kwa makofi na vifijo."

Watoto wa Gaza waliouawa na jeshi la Israel

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, fedheha ndilo neno dogo zaidi linaloweza kutumiwa kueleza hizaya na aibu hiyo ya Wamarekani.

Waziri Mkuu wa utawala bandia wa Israel jana alijitokeza katika Bunge la Congress la Marekani na kukariri madai yake ya uwongo. Hotuba ya Netanyahu imesusiwa na wawakilishi 128 wa Kongresi ya Marekani.

Tags