Sep 07, 2024 07:19 UTC
  • Araghchi asisitiza kuimarishwa uhusiano wa Iran na Serbia

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesitiza umuhimu wa kutumia rasilimali zote zilizopo ili kuimarisha uhusiano kati ya Iran na Serbia, hasa katika sekta ya uchumi.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo katika mazungumzo yakke kwa njia ya simu na Marko Duric Waziri wa Mashauri ya Serbia na kusisitiza uthabiti wa nchi za Balkan kama kipengele muhimu cha sera za kigeni za Iran.

Aidha Araghchi amesisitiza msimamo thabiti wa Iran katika kuunga mkono umoja wa ardhi yote ya Serbia na akaelezea upinzani dhidi ya mabadiliko yoyote ya mipaka au mienendo ya kijiografia ya kisiasa katika eneo hilo.

Bendera za Iran na Serbia

 

Wakati wa mazungumzo hayo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Serbia Marko Đurić amempongeza Abbas Araghchi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na kumtakia mafanikio mema katika nafasi yake mpya na kueleza matumaini kuwa ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili utaendelea kukua. Đurić alisifu ushirikiano unaoongezeka wa kiuchumi na akatoa mwaliko kwa sekta za biashara za Iran kushiriki kikamilifu katika Maonyesho ya EXPO 2027, yanayotarajiwa kufanyika Belgrade.

Kadhalika Mawaziri hao wa Mashauri ya Kigeni ya Iran na Serbia wamekubaliana, katika simu katika mazungumzo yao hayo kkwa njia ya simu juu ya  kuendelea na mashauriano kati ya nchi hizo mbili katika ngazi mbalimbali.

Tags